Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Saka nje wiki nane nyingine

Saka Pict

Muktasari:

  • Wakati Arsenal ikitangaza Mjerumani Kai Havertz atakuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu, matumaini ya kumshuhudia Saka uwanjani mapema yameyeyuka baada ya kuelezwa anaweza kuwa nje ya uwanja hadi katikati ya mwezi Aprili.

LONDON, ENGLAND: BUKAYO Saka ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki nane zaidi huku tatizo la majeruhi likiendelea kuwa kubwa na kusumbua kambi ya kikosi cha Arsenal.

Wakati Arsenal ikitangaza Mjerumani Kai Havertz atakuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu, matumaini ya kumshuhudia Saka uwanjani mapema yameyeyuka baada ya kuelezwa anaweza kuwa nje ya uwanja hadi katikati ya mwezi Aprili.

Saka aliumia kwenye mechi ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Crystal Palace, Desemba mwaka jana na kulikuwa na matumaini ya kurejea uwanjani mwezi ujao.

Hivi karibuni, klabu hiyo ilichapisha picha za mchezaji huyo akifanya mazoezi kwenye kambi yao huko Dubai, lakini sasa kinachoelezwa anakabiliwa na wiki nyingine nane nje ya uwanja.

Jambo hilo limeongeza pigo kubwa kwenye kikosi hicho cha Mikel Arteta, na sasa kitahitaji huduma ya Leandro Trossard, Raheem Sterling na kinda Ethan Nwaneri kuongoza kwenye safu yao ya ushambuliaji. Arteta anawakosa pia Wabrazili, Gabriel Jesus na Gabriel Martinelli.

Arsenal kwa sasa ipo nyuma kwa pointi saba dhidi ya vinara Liverpool kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya miamba hiyo ya Anfield kubanwa na Everton kwenye mchezo wao wa kiporo uliofanyika Goodison Park kwa kumalizika kwa matokeo ya mabao 2-2, Jumatano iliyopita.