Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Eto’o amgonga Geremi nyundo tano

ETOO Pict

Muktasari:

  • Geremi aliwahi kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka 2005 na 2006 wakati alipokuwa akiitumikia miamba hiyo ya Stamford Bridge. Alizichezea pia Middlesbrough, Newcastle na Real Madrid.

YAOUNDE, CAMEROON: STAA wa zamani wa Chelsea, Geremi Njitap amekumbana na nyundo ya kufungiwa soka miaka mitano huko Cameroon baada ya kutibuana na mchezaji mwenzake wa zamani, ambaye kwa sasa ni bosi, Samuel Eto’o.

Geremi aliwahi kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka 2005 na 2006 wakati alipokuwa akiitumikia miamba hiyo ya Stamford Bridge. Alizichezea pia Middlesbrough, Newcastle na Real Madrid.

Na hivi karibuni, Geremi, 46, alikuwa bosi wa chama cha wanasoka cha Cameroon, Synafoc.

Lakini, Chama cha soka cha nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Fecafoot, kimemfungia kujihusisha na soka hadi 2030 sambamba na kumpiga faini ya Pauni 13,000.

Staa wa zamani wa Chelsea, Everton, Barcelona na Inter Milan, Eto’o, 44, ndiye rais wa Fecafoot.

Malumbano yao yalianzia kwenye Afcon 2023 huko Ivory Coast, wakati Geremi aliporipotiwa kutibuana na mmoja wa maofisa wa Eto’o wakiwa kwenye vyumba vya kubadilishia.

Kamati ya nidhamu ya Fecafoot ilitangaza: “Tunatangaza Geremi Sorel Njitap, rais wa Synafoc, amekutwa na hatia ya utovu wa nidhabu na maadili. Tunamfungia kujihusisha na soka kwa miaka mitano na kulipa faini ya faranga milioni 10 (Pauni 13,000). Ana siku 10 za kuwasilisha rufaa yake kwa maandishi.”

Msaidizi wake Geremi, Daniel Blaise Ngos, naye amefungiwa miaka miwili na kutozwa faini ya faranga 6,500 kutokana na sakata hilo. Geremi aliichezea Cameroon mechi 118 na kufunga mabao 13.

Aliiwezesha nchi hiyo kushinda medali ya dhahabu kwenye Olimpiki 2000 na mataji mawili ya Afcon. Alishinda pia La Liga akiwa na Real Madrid mwaka 2001 na alicheza pia Paraguay, Uturuki na Ugiriki.

Aliachana na mkewe mwaka jana baada ya vipimo vya vinasaba kuonyesha watoto wawili aliozaa na mwanamke huyo hawakuwa wa kwake bali ni wa mpenzi wa zamani wa mwanamke huyo.