Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Eti Palmer atatua Old Trafford

Muktasari:

  • Meulensteen alisema kwa Palmer kuhamia Man United ni kitu kilichopo kwenye mipango yake na huenda hilo litatimia wakati atakapoamua kuachana na maisha ya Stamford Bridge.

LONDON, ENGLAND: ALIYEKUWA kocha wa kikosi cha kwanza cha Manchester United, Rene Meulensteen amefichua kwamba kuna siku moja kiungo wa Chelsea, Cole Palmer atakwenda kujiunga na miamba hiyo ya Old Trafford kwa sababu ndiyo timu anayoshabikia.

Meulensteen alisema kwa Palmer kuhamia Man United ni kitu kilichopo kwenye mipango yake na huenda hilo litatimia wakati atakapoamua kuachana na maisha ya Stamford Bridge.

Palmer, 23, alionyesha kiwango kizuri alipokuwa Manchester City kabla ya kuhamia Chelsea wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi 2023.

Akizungumza na Grosvenor Sport, Meulensteen alifunguka kuhusu staa huyo wa kimataifa wa England atakavyokwenda Old Trafford kukipiga huko siku moja.

Alisema: “Hii ni siri kwa jamii kwamba Cole Palmer ni shabiki wa Man United. Kitu kilichonishangaza ni Man United iliposhindwa kumchukua na kumfanya aende Manchester City na kisha Chelsea kumchukua.

“Palmer ni mchezaji anayeweza kuleta kitu tofauti uwanjani, na kwamba anaweza kwenda kujiunga Man United huko mbele? Ndio, sioni kwanini isiwe. Sawa, amesaini mkataba mrefu Chelsea, lakini wakati mwingine mambo hayaendi na wachezaji wanatibuana na klabu zao, hapo Man United inaweza kuvutiwa kumchukua. Ni shabiki wa Man United na ni mchezaji ambaye anaweza kuirudisha timu hiyo kwenye viwango vya juu.”

Meulensteen alikuwa kocha wa kikosi cha kwanza cha Man United kwa miaka sita chini ya kocha Sir Alex Ferguson hadi hapo gwiji huyo alipoondoka Old Trafford mwaka 2013. Palmer alifunga mabao 18 na asisti 14 kwenye michuano yote akiwa na kikosi cha Chelsea msimu uliopita.

Idadi hiyo ya mabao inahusisha pia matatu aliyofunga kuisaidia Chelsea kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu, ambapo Palmer alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa michuano hiyo.