Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Donnarumma ashtua mabosi Old Trafford

KIPA Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Old Trafford kwa sasa ipo sokoni kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kusaka kipa namba moja baada ya kutoridhishwa na kiwango cha kipa wa sasa, Andre Onana.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imepata mzuka baada ya kusikia kwamba kipa wa Paris Saint-Germain, Gianluigi Donnarumma anaweza kupatikana kwa bei ya kutupa.

Miamba hiyo ya Old Trafford kwa sasa ipo sokoni kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kusaka kipa namba moja baada ya kutoridhishwa na kiwango cha kipa wa sasa, Andre Onana.

Onana alijiunga na Man United kwa ada ya Pauni 47.1 milioni miaka miwili iliyopita, lakini amekumbana na wakati mgumu Old Trafford na sasa kinachoelezwa klabu inatafuta mbadala wake.

Man United imeonyesha dhamira kwa Donnarumma, 26, ambaye ameonekana kuwa na sintofahamu kuhusu mkataba wake mpya kwenye kikosi hicho cha mabingwa wa Ulaya. Donnarumma, anayehesabika kuwa mmoja wa makipa bora kabisa duniani kwa sasa, anaingia miezi 12 ya mwisho kwenye mkataba wake huko Parc des Princes. Na sasa, Man United imepata mzuka baada ya kusikia kwamba PSG inapanga bei ya Donnarumma kuwa Euro 40 milioni, kwa mujibu wa La Repubblica.

Kutokana na kwamba hakuna makubaliano ya kuongeza mkataba mpya yaliyofikiwa, huku ishu za kifedha zikiwa tatizo, klabu hiyo ya Ufaransa imefungua milango ya kumpiga bei dirisha hili. PSG itapenda kipa huyo Mtaliano abaki, lakini kinachoripotiwa ni kwamba inavutiwa na ofa inazopokea.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim anahitaji kipa mpya ambaye atakuwa namba moja na sasa kuna uwezekano mkubwa wa kupata saini ya Donnarumma.

Kwa mujibu wa L’Equipe, kipa huyo wa PSG amekuwa akiwaambia wachezaji wenzake kwamba anavutiwa na mpango wa kwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England. Lakini, anachosema Donnarumma kwa sasa: “Kipaumbele changu ni kubaki PSG. Sidhani kama kutakuwa na tatizo lolote juu ya kufikia makubaliano.”

Donnarumma alijiunga na PSG miaka mitano iliyopita akitokea AC Milan kwa uhamisho wa bure na tangu wakati huo amecheza mechi 154 za michuano yote akiwa na mabingwa hao wa Ufaransa. Man United pia inamfuatilia kipa wa Aston Villa, Emi Martinez.