Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Donnarumma anasubiri mlangoni Man United

Muktasari:


  • Miamba ya soka ya Italia, Inter Milan inataka kumrudisha Onana huko San Siro ikiwa ni miaka miwili imepita tangu ilipomuuza kwenda Man United. Onana amekuwa na panda shuka ya kiwango chake Man United tangu alipofika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alipokuwa na Inter mwaka 2023.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imepata tumaini jipya la kupata pesa kuiwezesha kumsajili Gianluigi Donnarumma kupitia Andre Onana anayesakwa na Inter Milan.

Miamba ya soka ya Italia, Inter Milan inataka kumrudisha Onana huko San Siro ikiwa ni miaka miwili imepita tangu ilipomuuza kwenda Man United. Onana amekuwa na panda shuka ya kiwango chake Man United tangu alipofika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alipokuwa na Inter mwaka 2023.

Alifanya makosa mengi msimu uliopita na hilo ndilo linalofanya Man United kutafuta kipa mwingine wa daraja la juu. Onana hakucheza mechi yoyote ya pre-season kutokana na kuwa majeruhi kabla ya kupona, lakini kocha Ruben Amorim hakumwaanzisha katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, Jumapili iliyopita. Amorim aliamua kumwaanzisha kipa Altay Bayindir na kumweka benchi Tom Heaton kwa kuwa ndiyo waliokuwa wakiidakia timu kwenye pre-season.

Man United imekuwa ikihusishwa na makipa wengi kama wabadala wa Onana. Na sasa kelele nyingi zinamtaja Gianluigi Donnarumma, ambaye mastaa wa zamani wa Man United wanaamini ndiye kipa anayestahili kwenye kukaa kwenye goli la timu hiyo, licha ya timu hiyo kumsaka pia Emi Martinez wa Aston Villa.

Senne Lammens naye yupo kwenye rada za Man United pamoja na Inter Milan.

Hata hivyo, kwa mujibu wa The Sun, Inter imeonyesha dhamira ya kumrudisha Onana kwenye timu yao huku kipa huyo Mcamerooni naye akifurahia hilo.

Kama Inter itapeleka ofa ya kumchukua Onana, hilo litairuhusu Man United kuwa na nguvu ya kumnasa kipa Donnarumma, licha ya kuivutia pia Manchester City. Kipa Mtaliano, Donnarumma alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita akiwa na kikosi cha Paris Saint-Germain, lakini atapatikana kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kwa Pauni 26 milioni tu baada ya miamba hiyo ya Ufaransa kunasa huduma ya kipa mwingine, Lucas Chevalier.