Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Arsenal kwa Gyokeres latibuliwa

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Arsenal iliripotiwa kuwa tayari imetoa ofa rasmi ya takribani pauni  62 milioni kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Sweden.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA inaripotiwa kuingilia dili la Arsenal kwa straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres iliyehitaji kumsajili katika dirisha hili.

Arsenal iliripotiwa kuwa tayari imetoa ofa rasmi ya takribani pauni  62 milioni kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Sweden.

Hata hivyo, kwa mujibu wa jarida la Record nchini Ureno, mahasimu wao wa London, Chelsea, sasa wameingia rasmi kwenye mbio za kumsaka mshambuliaji huyo.

Inaelezwa Chelsea wamewasilisha maombi rasmi ya kutaka kumnunua Gyokeres, hatua ambayo imekuja saa chache tu baada ya Chelsea kutwaa ubingwa wa UEFA Conference League kwa kuichapa Real Betis 4-1 huko Wroclaw, Poland.

Gyokeres mwenye umri wa miaka 26, amefunga mabao 97 na kutoa asisti 28 katika mechi 102 tangu ajiunge na Sporting kutoka Coventry mwaka 2023.

Msimu huu pekee, amefunga mabao 54 katika mashindano yote, na kumfanya kinara Ulaya, akiwapiku Kylian Mbappe na Robert Lewandowski ambao kila mmoja alifunga magoli 42.

Chelsea walikuwa wakingoja hadi baada ya fainali ya Conference League ili kuanza harakati zao rasmi kwenye soko la usajili.

Mabingwa hao wa Conference League sasa wanataka kukamilisha haraka usajili wa mshambuliaji mpya kabla ya kushiriki kwenye Kombe la Dunia la Klabu.

Nyota wa Ipswich Town, Liam Delap, pia yuko kwenye rada ya Chelsea, lakini anawindwa pia na Manchester United, Newcastle, na Everton.

Chelsea walifunga mabao 64 katika Ligi Kuu, wakiwa timu ya saba kwa mabao mengi msimu uliopita.

Wachezaji wanne walifunga mabao 10 au zaidi katika mashindano yote, lakini Cole Palmer na Nicolas Jackson tu ndio waliovuka mabaoi 10 kwenye ligi.

Kikosi cha Enzo Maresca kinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus, Man United na Arsenal katika harakati za kumnasa Gyokeres.

Hata hivyo, Chelsea ina orodha ndefu ya washambuliaji inaowataka ikiwa pamoja na Victor Osimhen, Benjamin Sesko na Hugo Ekitike.