Dembele bado ajifua kivyake

Muktasari:
- Staa huyo wa Paris Saint-Germain alikosa mechi ya kwanza ya timu yake ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani, wakati chama hilo lilipoichapa Atletico Madrid kwa mabao 4-0 na huenda akakosa mechi dhidi ya Botafogo.
LOS ANGELES, MAREKANI: WINGA Ousmane Dembele anaendelea kujifua kivyake wakati huu akipambana kupona maumivu ya misuli.
Staa huyo wa Paris Saint-Germain alikosa mechi ya kwanza ya timu yake ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani, wakati chama hilo lilipoichapa Atletico Madrid kwa mabao 4-0 na huenda akakosa mechi dhidi ya Botafogo.
Dembele aliumia alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa alipokitumikia kikosi cha Ufaransa.
Staa huyo bado hajapona na mwanzoni ilielezwa kwamba huenda angekosa mechi zote tatu za hatua ya makundi akiwa na kikosi cha PSG kwenye Kombe la Dunia la Klabu, ambapo hadi kufikia juzi Jumatatu alikuwa akifanya mazoezi kivyake kando na wenzake ambao wanapaswa pamoja.
Kama ilivyo kwa Dembele, PSG ilikosa huduma ya Bradley Barcola katika mechi ya kwanza baada ya kuumia pia wakati alipokuwa kwenye majukumu ya kuitumikia Les Bleus.
Staa huyo alipata maumivu kiasi kwenye goti, lakini alirejea kufanya na mazoezi na wenzake Jumatatu.
Kuna uwezekano mkubwa Barcola akarejea uwanjani Ijumaa, wakati PSG itakapokipiga na Botafogo. PSG itahitimisha hatua ya makundi kwa kukipiga na Seattle Sounders, Jumatatu.