Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dah! Maskini Andre Onana

ONANA Pict

Muktasari:

  • Nafasi ya makipa kwenye kikosi cha Man United kwa sasa ipo kwenye mashaka makubwa kutokana na kushindanisha makipa watatu, Onana, Altay Bayindir na Senne Lammens.

MANCHESTER, ENGLAND: USIOMBEE kuchokwa. Hicho ndicho kinachomkuta kipa Andre Onana kwa sasa baada ya mashabiki wa Manchester United kuwataka mabosi wa timu hiyo kukubali haraka ofa ya kumpiga bei nyanda huyo wa Cameroon.

Nafasi ya makipa kwenye kikosi cha Man United kwa sasa ipo kwenye mashaka makubwa kutokana na kushindanisha makipa watatu, Onana, Altay Bayindir na Senne Lammens.

Bayindir ameanzishwa kwenye mechi zote tatu ilizocheza Man United kwenye Ligi Kuu England, huku Onana alidaka mechi ya Kombe la Ligi, ambapo timu hiyo ilipoteza na kutupwa nje ya michuano dhidi ya timu ndogo ya League Two, Grimsby.

ONA 01

Kipa Lammens amejiunga na Man United kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili, akionekana kwenda kuchukua namba moja golini, huku mchakato huo ukifungua milango ya Onana kuondoka baada ya timu za Uturuki kuhitaji huduma yake.

Trabzonspor imeonyesha dhamira ya kunasa saini ya kipa Onana na huenda ikapeleka maombi ya kumchukua kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili huko Uturuki halijafungwa Septemb 12.

Na mashabiki wa Man United sasa wamewaambia mabosi wao, ofa ya Onana ikiletwa wakubali haraka ili kipa huyo aondoke baada ya kuwakera kwa namna alivyoruhusu mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Grimsby.

Shabiki mmoja alisema: "Mkubali hiyo ofa haraka."
Mwingine aliongeza: "Hallelujah. Uturuki iwe mwokozi."
Shabiki wa tatu alisema: "Hebu tufanye huo uhamisho uwe wa jumla tafadhali."

ONA 02

Na shabiki mwingine alisema: "Chukueni dili hilo."
Kiwango cha Onana kimekuwa kikikosolewa sana kwa miaka yote miwili tangu alipojiunga na Man United. Alikosa mechi za kwanza za ligi kutokana na kuwa majeruhi na mechi ya tatu aliishia kukaa benchi wakati Man United ilipoichapa Burnley 3-2 kwenye Ligi Kuu England.

Lammens anaweza kuwa kipa namba moja wa Man United baada ya kusajili kwa Pauni 18 milioni na kusaini mkataba wa miaka mitano huko Old Trafford.