Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cunha awashusha presha Man United

CUNHA Pict

Muktasari:

  • Cunha alipata maumivu ya misuli katika mechi hiyo jambo lililomfanya kocha Ruben Amorim kuwa kwenye wakati mgumu kutokana na mkali huyo wa Kibrazili alivyoanza kwa moto msimu huu katika kikosi chake kipya cha huko Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA mpya wa Manchester United, Matheus Cunha amesema atakuwa fiti na kurejea uwanjani hivi karibuni baada ya kushindwa kuendelea na mchezo kwenye ushindi dhidi ya Burnley katika mchakamchaka wa Ligi Kuu England, Jumamosi iliyopita.

Cunha alipata maumivu ya misuli katika mechi hiyo jambo lililomfanya kocha Ruben Amorim kuwa kwenye wakati mgumu kutokana na mkali huyo wa Kibrazili alivyoanza kwa moto msimu huu katika kikosi chake kipya cha huko Old Trafford.

Cunha alisajiliwa kutokea Wolves kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka huu na alionekana kuwa moto huko Man United akitafuta bao lake la kwanza.

Hata hivyo, maumivu ya misuli ilimfanya kutolewa kwenye kipindi cha kwanza wikiendi iliyopita. Cunha aliondoka mwenyewe bila ya msaada wowote baada ya mechi hiyo na hivyo kuamsha matumaini makubwa kwamba majeraha yake si makubwa sana na atarudi uwanjani hivi punde.

Baada ya kuwekwa nje kwenye kikosi cha Brazili, Cunha alisema: "Hilo ni jambo bora kabisa, najisikia vizuri kabisa. Nitarudi uwanjani hivi karibuni. Asante kwa meseji zenu."

Kocha Amorim alikuwa na wasiwasi pia kuhusu hali ya kiungo wake mwingine, Mason Mount, aliposema: "Ni kitu kigumu kukosa wasiwasi unapompoteza mchezaji kama Cunha na Mason Mount. Mount alicheza dakika 30 akiwa na maumivu. Sifahamu kama ni majeraha ya muda mrefu, sifahamu, lakini yananifikirisha. Ni wachezaji muhimu kwetu, ngoja tuone."

Man United imekusanya pointi nne katika mechi tatu ilizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu huku mechi yao ijayo ni ya kuwakabili mahasimu wao wakuu, Manchester City huko uwanjani Etihad. Katika mechi hiyo, Man United itahitaji kuwa na kikosi chake chote kikiwa kamili ili kutafuta ushindi muhimu kutoka kwenye uwanja wa majirani zao hao.