Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Comeback yaipa Korea Kusini pointi tatu muhimu Kombe Dunia

Muktasari:

  • Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Guadarajala, Mexico, umezifanya timu zote kumaliza dakika 45 za kwanza zikiwa hazijafungana, huku zikishambuliana kwa hesabu.

Korea Kusini imetoka nyuma na kwenda kutengeneza ushindi, ikiichapa Jamhuri ya Czech kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa pili wa Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Guadarajala, Mexico, umezifanya timu zote kumaliza dakika 45 za kwanza zikiwa hazijafungana, huku zikishambuliana kwa hesabu.

Czech ikawa ya kwanza kupata bao dakika ya 59 kupitia beki Ladislav Krejci anayeichezea Wolves ya England aliyemalizia pasi ya mwenzake Vladimir Koufal.

Dakika nane baadaye Korea Kusini imefanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa kiungo Hwang In- Beom anayeichezea Feyernoord ya Uholanzi, akimalizia vizuri pasi ya Lee Kang- In.

Bao hilo likaiongezea nguvu Korea Kusini ikiandika bao la pili dakika ya 80 mfungaji akiwa Oh Hyeon -Gyu akimalizia asisti ya mfungaji wa bao la kwanza Hwang In- Beom.

Ushindi huo unaifanya Korea Kusini kushika nafasi ya pili kwenye kundi A linaloongozwa na wenyeji, Mexico, ambao walitangulia kuifunga Afrika Kusini kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi.

Mchezo huo umeshuhudiwa ukiamuliwa na mwamuzi wa kwanza kutoka Afrika, Amin Mohamed Omar ambaye ni raia wa Misri.