Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea kujiweka pabaya Marekani

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha kocha Enzo Maresca kilisambaratishwa na wababe hao wa Brazil baada ya kuchapwa 3-1 huko Philadelphia. Kipigo hicho kina maana Chelsea haina uhakika wa kuongoza kundi lake, kutokana na Flamengo kuwa na pointi tatu na mabao manne zaidi ya wapinzani wao.

PHILADELPHIA, MAREKANI: CHELSEA ipo kwenye hatari ya kupangwa na timu ngumu kwenye hatua ya mtoano baada ya kupoteza dhidi ya Flamengo, Ijumaa iliyopita.

Kikosi hicho cha kocha Enzo Maresca kilisambaratishwa na wababe hao wa Brazil baada ya kuchapwa 3-1 huko Philadelphia. Kipigo hicho kina maana Chelsea haina uhakika wa kuongoza kundi lake, kutokana na Flamengo kuwa na pointi tatu na mabao manne zaidi ya wapinzani wao.

Chelsea bado inaweza kutinga hatua ya 16 bora endapo kama itakwepa kipigo dhidi ya ES Tunis usiku wa kuamkia Jumatano. Hata hivyo, jambo hilo linaweza kuwaweka kwenye wakati mgumu katika raundi ya 16.

Timu inayoshika nafasi ya pili kwenye kundi la Chelsea itacheza na timu itakayoongoza Kundi C kwenye mtoano huo. Na hapo, huenda ikakumbana na Bayern Munich ya straika Harry Kane, ambao kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia la Klabu imeshazifunga Auckland City na Boca Juniors.

Mechi hiyo ngumu itafanyika Charlotte kwenye Uwanja wa Bank of America, Juni 28.

Bayern inaweza kushindwa kuongoza kundi lao, endapo kama Benfica itawachapa Jumanne.

Kama Chelsea itavuka na kutinga robo fainali, kuna nafasi kubwa ikaenda kukabiliana na mabingwa wa Ulaya, Paris Saint-Germain, ambayo iliduwazwa mapema wiki iliyopita, ilipochapwa 1-0 na Botafogo.

Hilo linaloifanya PSG kuwa na uwezekano wa kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi B. Kama hilo likitokea, basi miamba hiyo ya Ufaransa itakabiliana na timu itakayoongoza Kundi A na inaweza kuwa Palmeiras au Inter Miami, kwenye raundi ya 16 bora - kabla ya kuwapo kwa uwezekano wa kucheza na Chelsea.