Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick afichua mpango wa kusuka upya kikosi

CARRICK Pict

Muktasari:

  • United tayari wamepoteza kiungo muhimu Casemiro ambaye anaondoka na wanatarajiwa kuwaacha Marcus Rashford, Andre Onana, Manuel Ugarte, Joshua Zirkzee pamoja na Rasmus Hojlund katika mchakato wa kujenga upya kikosi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick amesema klabu hiyo lazima iendelee kusonga mbele dirisha muhimu la usajili wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa.

Carrick alipewa kazi ya ukocha wa kudumu baada ya kuiwezesha United kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England na kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), baada ya kuchukua nafasi ya Ruben Amorim aliyefutwa kazi Januari.

United tayari wamepoteza kiungo muhimu Casemiro ambaye anaondoka na wanatarajiwa kuwaacha Marcus Rashford, Andre Onana, Manuel Ugarte, Joshua Zirkzee pamoja na Rasmus Hojlund katika mchakato wa kujenga upya kikosi.

“Nafikiri kila dirisha la usajili huonekana kuwa muhimu zaidi duniani kwa kila klabu,” alisema Carrick.

“Kama klabu tunataka kuendelea mbele. Tunaelewa bado kuna kazi kubwa ya kufanya, hasa kutokana na baadhi ya wachezaji kuondoka.”

Carrick pia alisema amefurahishwa na maendeleo ya vijana wa timu hiyo akiwemo Kobbie Mainoo, Amad Diallo, Ayden Heaven na Leny Yoro.

“Nimeona maendeleo makubwa. Wachezaji wanakua kiufundi na kiakili. Mafanikio huwafanya wajiamini zaidi.”

Kiungo huyo alishanukuliwa akisema United inahitaji zaidi ya wachezaji watano wapya kwenye kikosi hicho ili kiwe kwenye kasi kubwa msimu ujao wa ligi ambao mabosi wa timu hiyo wanataka mafanikio makubwa zaidi ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Kabla ya mechi ya jana ya kufunga msimu United ilikuwa na pointi 68 baada ya kucheza michezo 37 ya ligi hiyo.