Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher aomba radhi utata makipa bora

Muktasari:

  • Kipa huyo wa zamani wa Manchester United, Van der Sar alitumia zaidi ya miaka mitano Old Trafford, akitwaa mataji manne ya Ligi Kuu England, anachukuliwa kuwa miongoni mwa makipa bora zaidi katika historia ya ligi hiyo.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa zamani wa Ligi Kuu England, Jamie Carragher amelazimika kuomba radhi baada ya kumweka Edwin van der Sar nje ya orodha yake ya makipa watano bora wa wakati wote wa Ligi Kuu England, huku Mdachi huyo akimkosoa moja kwa moja katika studio za Sky Sports.

Kipa huyo wa zamani wa Manchester United, Van der Sar alitumia zaidi ya miaka mitano Old Trafford, akitwaa mataji manne ya Ligi Kuu England, anachukuliwa kuwa miongoni mwa makipa bora zaidi katika historia ya ligi hiyo.

Hata hivyo, Carragher alimweka katika nafasi ya sita kwenye orodha ya makipa bora wa muda wote, akimtanguliza juu ya wachezaji kama Ederson na David Seaman, ambao pia walitwaa mataji kadhaa ya ligi.

Van der Sar alitania alipoiona orodha hiyo: “Nilidhani ningeingia kwenye tano bora Jamie, jamani!”

Beki huyo wa zamani wa Liverpool alidai kuwa Van der Sar alikuwa kwenye tano bora hadi walipofanya mzaha kuhusu kutoshinda kwake ligi.

“Ulikuwepo kwenye tano bora hadi uliposema sijashinda Ligi Kuu England,” alisema Carragher na kuongeza. “Ulichokifanya Man United kilikuwa cha ajabu sana na naomba radhi, lakini, Gary Neville alielezea vizuri zaidi kuliko mimi. Ulipokuja, Man Utd ilianza kushinda mataji tena na kufika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.”

Makipa wengine wawili wa zamani wa Man United pia waliorodheshwa, huku David de Gea, aliyesajiliwa kuchukua nafasi ya Van der Sar, akishika nafasi ya nne. Peter Schmeichel, anayechukuliwa na wengi kama kipa bora zaidi katika historia ya Ligi Kuu England, aliwekwa nafasi ya pili na Carragher. Mchambuzi huyo wa Sky Sports alimuweka Thibaut Courtois katika nafasi ya tano, Mbelgiji huyo akitwaa mataji mawili ndani ya miaka minne akiwa na Chelsea.

Alisson Becker alikuwa chaguo lake la tatu, lakini kipa wa zamani wa Chelsea, Petr Cech alishika nafasi ya kwanza. Alikuwa muhimu sana katika utawala wa mapema wa Jose Mourinho katika Uwanja wa Stamford Bridge na bado anashikilia baadhi ya rekodi bora za ulinzi katika historia ya Ligi Kuu England.

Carragher alisema: “Sikuweza kusahau kabisa kiwango cha Petr Cech kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich. Nilikuwa uwanjani usiku huo. Aliwaweka Chelsea kwenye mchezo ule na hatimaye akawasaidia kuushinda. Nilicheza dhidi yake mara nyingi sana. Ulikuwa unaingia uwanjani na kujiuliza, ‘Tutafungaje dhidi yake?’.”