Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher anasema Salah kapewa ofa

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Anfield alisema angeshangaa sana kama mabosi wa Liverpool wasingempa ofa tamu Mo Salah kutokana na kiwangio chake anachoonyesha kwa sasa huku mkataba wake wa sasa ukielekea ukingoni.

LIVERPOOL, ENGLAND: JAMIE Carragher amefichua kwamba Liverpool tayari imeshampa ofa ya mkataba mpya Mohamed Salah.

Gwiji huyo wa Anfield alisema angeshangaa sana kama mabosi wa Liverpool wasingempa ofa tamu Mo Salah kutokana na kiwangio chake anachoonyesha kwa sasa huku mkataba wake wa sasa ukielekea ukingoni.

Hatima ya kinara huyo wa mabao na asisti kwenye Ligi Kuu England bado haifahamiki baada ya kubakiza miezi minne tu kwenye mkataba wake wa sasa.

Wakati Liverpool ikipasua kichwa kwa mchezaji huyo atakayetimiza miaka 33 mwishoni mwa msimu huu, Carragher haoni kama ni shida kumpa dili refu Mo Salah kutokana na ubora wake wa sasa.

"Msimwamini anavyosema kwamba hakupewa ofa ya mkataba mpya. Ninachoweza kuwahakikishia kwamba amepewa ofa ya mkataba mpya,” alisema Carragher.

Akizungumza na Paul Scholes, ambaye ni staa wa zamani wa Manchester United, alisema: "Unapofikisha miaka zaidi ya 30 timu nyingi zinajiuliza na hivyo ndivyo ilivyo. Lakini, siku hizi mambo ni tofauti. Zama zetu zile unapofika miaka 35 kwisha habari, ila siku hizi unaona mchezaji hadi wa miaka 37, 38, 39, 40."

Mo Salah ameibua wasiwasi kwa mashabiki wa Liverpool baada ya kudai kwamba mabosi wa timu hiyo bado hawajampa ofa ya mkataba mpya, wakati mkataba wake wa sasa ukifika tamati mwisho wa msimu huu, sawa na ilivyo kwa wakali wengine wa miamba hiyo ya Anfield, Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold.