Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher akataa usajili wa Isak

ISAK Pict

Muktasari:

  • Straika Isak, 25, amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Anfield baada ya kutangaza dhamira yake ya kuachana na Newcastle United.

LIVERPOOL, ENGLAND: GWIJI wa Liverpool, Jamie Carragher amewaambia mabosi kufuta mpango wa kumsajiliAlexander Isak.

Straika Isak, 25, amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Anfield baada ya kutangaza dhamira yake ya kuachana na Newcastle United.

Kwa sasa staa huyo anathaminishwa na Newcastle kuwa na thamani ya Pauni 150 milioni na kwamba mabosi wa St James’ Park wanan-g’ang’ania kulipwa kiwango hicho cha pesa. Lakini, beki wa zamani wa Liverpool, Carragher alisema: “Nikiwa kama shabiki wa Liverpool maoni yangu ni kwamba timu isitumie Pauni 150 milioni kwa ajili ya kumsajili Isak. Unashindwa kuelewa Liverpool isajili straika mwingine wa zaidi ya Pauni 80 milioni na ni chaguo la pili. Hii kitu haiko sawa.”

Carragher ametoa hoja hiyo hasa ukizingatia Liverpool imetumia pesa nyingi dirisha hili kunasa saini ya straika Hugo Ekitike, kutoka Eintracht Frankfurt kwa Pauni 79 milioni.

Gwiji huyo anaamini usajili wa Isak sio wa mipango na umeibuka  baada ya kuona kuna fursa ya kuweza kupata saini yake baada ya kutangaza anataka kuachana na timu yake.

Carragher aliongeza: “Natazama huu usajili wa Isak kama ni mchezo tu. Hauonekani kuwa uliandaliwa. Kwa sababu huwezi kununua straika kwa Pauni 80 milioni, kisha unataka kununua straika mwingine kwa Pauni 120 milioni.

“Sitaki Liverpool imsajili, lakini Pauni 150 milioni kwangu naona kama vile anasajiliwa Kylian Mbappe, unaweza kumpata Mbappe kwa Pauni 150 milioni.”

Licha ya kumjumuisha Ekitike kwenye kikosi Liverpool bado ina pesa ya kutosha baada ya kumuuza Darwin Nunez huko Al Hilal kwa Pauni 46 milioni, hivyo itahitaji mshambuliaji mwingine.