Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Canada yashindwa kutamba nyumbani ikilazimishwa sare

Muktasari:

  • Canada imeshindwa kupata ushindi wake wa kwanza katika Fainali za Kombe la Dunia baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bosnia&Herzegovina

Timu ya Taifa ya Canada imeshindwa kutamba kwenye ardhi yake ya nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bosnia&Herzegovina.

Canada ambao ni waandaaji wenza wa Kombe la Dunia wakishirikiana na Marekani na Mexico, ndio walikuwa wa kwanza kuruhusu nyavu zao kutikiswa dakika ya 21 kwa bao la  mchezaji wa Bosnia&Herzegovina, Jovo Lukic aliyefunga kwa kichwa  akimalizia mpira wa kona  wa Sead Kolasinac.

Wenyeji walijaribu kufanya mashambulizi kadhaa kurejea mchezoni hadi ilipofika dakika ya 78 waliposawazisha kupitia kwa Cyle Lerin aliyefunga kwa kumalizia pasi nzuri ya Promise David.

Hata hivyo, jitihada za kupata bao la ushindi ziligonga mwamba kwa kila timu na kuifanya Canada kuendelea kutopata ushindi katika mashindano hayo makubwa duniani.

Licha ya shangwe kubwa la takribani mashabiki  45,000 waliokuwa wameujaza uwanja wa BOM jijini Toronto, hawakuweza kushuhudia Canada ikipata ushindi kwenye ardhi ya nyumbani wakisubili uwezekano wa kupata ushindi wao wa kwanza katika mechi inayofuata ambapo watavaana na wenyeji wa michuano iliyopita ya mwaka 2022, Qatar, Juni 19.

Canada imecheza bila uwepo wa nyota wake mkubwa Alphonso Davis kwa vile nahodha huyo anasumbuliwa na majeraha ya misuli.

Hata hivyo, nyota wengine kama Jonathan David na Stephen Eustaquiro walionyesha mchango kuhakikisha timu hiyo inaondoka bila kupoteza mchezo.

Kwa upande wa Bosnia&Herzegovina yenyewe ilimkosa nyota wake mkongwe Edin Dzeko ambaye amefunga mabao sita katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2026. Nahodha huyo amekosekana kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Mchezo mwingine wa kundi B utachezwa Jumamosi saa 4:00 usiku ukizikutanisha Switzerland dhidi ya Qatar.