Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bilionea wa Qatar aipotezea Man United

Muktasari:

  • Aidha, taarifa zinaeleza kuwa hata kama mawasiliano hayo yangefanyika, ni jambo lisilowezekana kwa sasa kwa kundi hilo kuwasilisha ofa mpya ya kuinunua Manchester United.

LONDON, England: KUNDI la wawekezaji kutoka Qatar ambalo hapo awali lilishindwa kuinunua klabu ya Manchester United halijawasiliana maombi mengine kuhusu uwezekano wa kuinunua klabu hiyo, licha ya ripoti zinazoeleza kuwa familia ya Glazer family inafikiria kuiuza hisa zake.

Aidha, taarifa zinaeleza kuwa hata kama mawasiliano hayo yangefanyika, ni jambo lisilowezekana kwa sasa kwa kundi hilo kuwasilisha ofa mpya ya kuinunua Manchester United.

Kwa muda mrefu kumekuwa na uvumi kwamba familia ya Glazer, yenye makazi yake Florida nchini Marekani, inatafakari kumaliza utawala wake wa miaka 21 katika uwanja wa Old Trafford na kuuza hisa zake.

Ripoti ya Bloomberg ilidai kuwa baadhi ya wanafamilia wa Glazer wanataka kuondoka na wanajaribu kuwashawishi wengine kufanya hivyo pia. Manchester United imekataa kutoa maoni kuhusu taarifa hiyo, huku vyanzo vya juu ndani ya klabu vikikanusha kwa nguvu madai hayo. Familia ya Glazer, ambayo kwa kawaida huwa haizungumzii masuala yake hadharani, haikupatikana kwa maoni. Mwaka 2023, kundi la wawekezaji kutoka Qatar lililoongozwa na Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani liliwasilisha ofa ya kuinunua Manchester United baada ya familia ya Glazer kukaribisha zabuni kutoka kwa wanunuzi.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa hadi sasa kundi hilo halijawahi kuwasiliana rasmi wala kwa njia isiyo rasmi ili kupimwa kama bado lina nia ya kuinunua klabu hiyo.

Iwapo hali hiyo ingebadilika, inatarajiwa kuwa juhudi zozote za kuwashawishi warejee mezani kwa ofa mpya zingekataliwa haraka.

Kundi hilo bado lina maumivu kutokana na mchakato wa miaka mitatu iliyopita. Liliwasilisha ofa ya mwisho ya takribani pauni5 bilioni  kwa ajili ya kupata umiliki kamili wa klabu, lakini familia ya Glazer ilichagua kuuza asilimia 25 ya hisa zake kwa Sir Jim Ratcliffe kwa pauni 1.3 bilioni badala yake. Kwa sasa, kundi hilo la Qatar halina mpango wowote wa kurejea katika mazungumzo ya kuinunua Manchester United.

Baada ya uwekezaji wa Ratcliffe kupitia kampuni ya INEOS, alikabidhiwa usimamizi wa shughuli za kila siku za klabu. Mara moja alianza mchakato mkubwa wa mapitio ya biashara ya klabu, ambao ulijumuisha kupunguza mamia ya wafanyakazi na kubana matumizi.

Taarifa za hivi karibuni za kifedha za Manchester United zinaonyesha kuwa klabu ilipata faida ya uendeshaji ya pauni37.7 milioni katika kipindi cha miezi tisa kilichoishia Machi.