Benzema atetewa EURO 2020

Monday June 21 2021
benzema pic

BARCELONA, HISPANIA. KARIM Benzema, 33, alirudishwa kwa mbwembwe kwenye timu ya taifa ya Ufaransa ili kuisaidia katika Kundi la Kifo la Euro 2020 baada ya kutengwa na kocha Didier Deschamps kwa miaka sita. Lakini tangu amerejea hajafanya kilichotarajiwa na staa wa timu hiyo, Antoine Griezmann, amejitokea kumkingia kifua.

“Benzema akifunga bao moja tu mengine yatakuja,” alisema Griezmann kuhusu staa huyo ambaye alikuwa na kiwango bora kabisa Real Madrid, ambako alifunga mabao 30 katika mechi 46.

Advertisement