Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benjamin Sesko ishu ipo patamu

SESKO Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya St James’ Park inamtazama staa huyo wa RB Leipzig kama mchezaji mbadala wa kwenda kuchukua mikoba ya straika Alexander Isak.

NEWCASTLE, ENGLAND: NEWCASTLE United imeboresha ofa yao ya Pauni 70 milioni kwa ajili ya kuhakikisha inaipiku Manchester United kwenye mchakamchaka wa kufukuzia huduma ya straika Benjamin Sesko.

Miamba hiyo ya St James’ Park inamtazama staa huyo wa RB Leipzig kama mchezaji mbadala wa kwenda kuchukua mikoba ya straika Alexander Isak.

Lakini, inafahamu wazi Man United nayo inamtaka mchezaji huyo baada ya kocha Ruben Amorim kutaka kuboresha safu ya ushambuliaji ya timu yake.

Newcastle inataka kuweka rekodi ya klabu ya uhamisho kwa straika huyo wa kimataifa wa Slovenia, ambaye alifunga mabao 21 na asisti sita msimu uliopita.

Lakini, baada ya kuripotiwa mchezaji mwenyewe amefungua milango ya kujiunga na timu hiyo, Newcastle sasa imeweka mezani ofa ya Pauni 70 milioni na ziada ya Pauni 8.4 milioni, kufanya dau lote kufikia Pauni 78.4 milioni kwa ajili ya kunasa saini ya mkali huyo.

Man United bado haijapeleka ofa kwa ajili ya Sesko, licha ya kwamba mchezaji mwenyewe amekubali kwenda kukipiga Old Trafford.

Kutokana na presha hiyo, Newcastle imeamua kuongeza pesa huku ikisubiri jibu la mwisho ndani ya saa 24, kama itashindikana basi wafikirie wachezaji wengine endapo kama Sesko atachagua kujiunga na Man United.

Newcastle imefarijika na majibu ya RB Leipzig, baada ya David Ornstein kudai kwamba miamba hiyo ya Ujerumani kwa sasa itapendelea zaidi Sesko kwenda Newcastle kutokana na hali ilivyo kwa sasa kwa mkwanja uliowekwa mezani.

Dili hilo litakuwa habari njema kwa straika Isak, anayetaka kwenda Liverpool.

Liverpool ipo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza endapo itapata uhakika wa Isak kupatikana sokoni.

Man United inaweza kupindua meza hasa kwa kipindi hiki ikihitaji saini ya Sesko kwenda kuungana na mastaa wengine wapya Matheus Cunha na Bryan Mbeumo kwenye safu ya ushambuliaji ya miamba hiyo inayonolewa na Amorim.