Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beckham afunguka ishu ya mwanaye

Muktasari:

  • Brooklyn, mzaliwa wa kwanza kati ya watoto wanne wa David na Victoria Beckham, alitoa tamko la kushtua kupitia mitandao ya kijamii akiwashambulia wazazi wake, familia yao, na jinsi walivyomtendea mke wake, mrembo Nicola Peltz.

MIAMI, MAREKANI: DAVID Beckham amezungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu mwanawe Brooklyn atoe madai makubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mgogoro wa familia hiyo ya kitajiri.

Brooklyn, mzaliwa wa kwanza kati ya watoto wanne wa David na Victoria Beckham, alitoa tamko la kushtua kupitia mitandao ya kijamii akiwashambulia wazazi wake, familia yao, na jinsi walivyomtendea mke wake, mrembo Nicola Peltz.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema kuwa wazazi wake wamekuwa wakijaribu kumdhibiti kwa sehemu kubwa ya maisha yake ili kulinda kile alichokiita “Brand Beckham”. Brooklyn pia alimshutumu mama yake kwa kuvuruga harusi yake kimakusudi zaidi ya mara moja, ikiwemo dansi aliyodai haikuwa ya kufaa, na kusisitiza kuwa “hataki maridhiano” na familia yake.

Na sasa Beckham alizungumza katika kipindi cha kifedha cha CNBC kiitwacho Squawk Box, ambapo alizungumzia kuhusu makosa ambayo watoto wanaweza kufanya kupitia mitandao ya kijamii.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na England alisema: “Nimekuwa nikizungumza mara kwa mara kuhusu mitandao ya kijamii na nguvu iliyonayo, iwe kwa mazuri na kwa mabaya. Kile ambacho watoto wanaweza kufikia siku hizi kinaweza kuwa hatari.

“Lakini, kwa uzoefu wangu binafsi, hasa kwa watoto wangu, ni muhimu kuitumia mitandao kwa njia sahihi. Nimeweza kutumia jukwaa langu kuwafikia watu kwa ajili ya UNICEF. Na limekuwa chombo kikubwa sana cha kuwafanya watu watambue yanayotokea duniani kuhusu watoto.”

Beckham, ambaye alizichezea pia Inter Milan, Paris Saint Germain na LA Galaxy aliongeza: “Nimejaribu kufanya vivyo hivyo kwa watoto wangu, kuwaelimisha. Wanafanya makosa, lakini watoto wanaruhusiwa kufanya makosa. Hivyo ndivyo wanavyojifunza. Hilo ndilo ninalojaribu kuwafundisha watoto wangu. Wakati mwingine unapaswa kuwaacha wafanye makosa hayo pia.”

Kauli hizo zilikuja baada ya Beckham kukabiliwa na maswali mengi ya waandishi wa habari alipokuwa akipiga picha katika Mkutano wa 56 wa Uchumi Duniani (World Economic Forum) uliofanyika Davos, Uswisi.