Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern yambeba bure Jonathan Tah

JONATHAN Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani, baada ya kuhusishwa na Barcelona kwa sehemu kubwa ya msimu huu, ameamua kujiunga na Bayern akisaini mkataba hadi mwaka 2029.

MUNICH, UJERUMANI: KATIKA maandalizi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA, Bayern Munich imefanikiwa kumsajili Jonathan Tah kwa uhamisho wa bure kutoka Bayer Leverkusen.

Beki huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani, baada ya kuhusishwa na Barcelona kwa sehemu kubwa ya msimu huu, ameamua kujiunga na Bayern akisaini mkataba hadi mwaka 2029.

Baada ya kusaini mkataba huo, Tah mwenye umri wa miaka 29, alisema: “Nimefurahi sana kuwa FC Bayern. Nataka kuchukua majukumu hapa na kufanya kazi kwa bidii kila siku ili tufanikishe kama timu na kushinda mataji mengi pamoja.”

Wakati huohuo, Christoph Freund, mkurugenzi wa michezo wa Bayern, alisema: “Hakika kwa Jonathan Tah tumepata mchezaji mwenye uzoefu wa kimataifa na ubora, ambaye hatahitaji muda mrefu kujiweka imara katika ulinzi wetu. Atakuwa msaada mzuri na mchezaji muhimu kwetu kutokana na ubora wake wa kiufundi pamoja na tabia yake na jinsi anavyoongoza wenzake.”

Naye Mkurugenzi wa Soka wa Bayern, Max Eberl, aliongeza: “Sio siri, tumekuwa tukimfuatilia Jonathan Tah kwa muda mrefu. Tunathamini ubora wake, ni mtu mwenye tabia ya kuchukua majukumu.

“Jonathan alikuwa na ofa nyingi lakini ameichagua FC Bayern jambo ambalo linatufurahisha sana.”

Bayern kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA itakayoanza Juni 14 hadi Julai 13, 2025 nchini Marekani ikishirikisha timu 32, huku mabingwa hao wa Ujerumani wakipangwa Kundi C na timu za Auckland City (Marekani), Boca Juniors (Argentina) na Benfica (Ureno).