Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern yakwaa kisiki, Augsburg yaitibulia

Muktasari:

  • Beki wa Kijapani Hiroki Ito aliipa Bayern uongozi katikati ya kipindi cha kwanza kwa mpira wa kichwa, lakini mabao ya Arthur Chaves na Han-Noah Massengo ndani ya dakika 15 za mwisho yaliwapa wageni ushindi.

BAADA ya Bayern Munich kucheza mechi 27 mfululizo bila kupoteza katika Bundesliga, rekodi hiyo  imefikia mwisho wa ghafla jioni hii ya  Jumamosi baada ya Augsburg, waliokuwa wakihangaika, kupata ushindi wa kushangaza kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Beki wa Kijapani Hiroki Ito aliipa Bayern uongozi katikati ya kipindi cha kwanza kwa mpira wa kichwa, lakini mabao ya Arthur Chaves na Han-Noah Massengo ndani ya dakika 15 za mwisho yaliwapa wageni ushindi.

Hicho ni kipigo cha kwanza katika Ligi kwa Bayern msimu huu na kilionekana kutowezekana pale Ito alipofunga kwa kichwa kutoka kona ya Michael Olise dakika ya 23 na kumpa winga huyo wa zamani wa Crystal Palace pasi yake ya 14 ya mabao msimu huu, nyingi zaidi katika Bundesliga.

Hata hivyo, Bayern ilionekana dhaifu isivyo kawaida katika ulinzi na ilikuwa na bahati kwamba shuti kali la Robin Fellhauer katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza liligonga mwamba wa lango.

Iwapo hilo lilikuwa onyo kwa kikosi cha Vincent Kompany, halikutiliwa maanani.

Dakika chache baada ya Elvis Rexhbecaj kupiga shuti lililopita juu ya lango akiwa anaelekea kufunga, Chaves alimshinda kipa wa Bayern, Jonas Urbig kwa kufika kwanza katika kona na kupiga kichwa mpira uliotumbukia kwenye lango lililoachwa wazi.

Urbig alianza badala ya Manuel Neuer aliyepumzishwa, ikiwa ni moja ya mabadiliko manne aliyofanya Kompany, lakini hakuwahi kuonekana mwenye kujiamini.

Baada ya kupoteza michezo yote minane waliyokuwa nyuma kwa mabao msimu huu,  Augsburg waliibuka kwa kugeuza matokeo wakati Massengo alipomalizia kwa ustadi shambulizi zuri la pamoja dakika tisa kabla ya mwisho na kuwashangaza  watetezi hao.

Bayern walishambulia kwa nguvu kutafuta bao la kusawazisha, lakini Olise ambaye sasa ana mabao manne na pasi saba za mabao katika michezo yake mitano ya mwisho ya ligi, alipiga shuti la mbali lililogonga mtambaa wa lango katika mpira wa mwisho wa mchezo.

Harry Kane alikuwa na mchana mtulivu na hakusaidia Bayern kufunga angalau mabao mawili, ambayo yangewapa rekodi mpya ya michezo 27 mfululizo ya Bundesliga.

Licha ya kipigo hiki cha kushangaza, Bayern wanasalia kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na tofauti ya pointi 11 dhidi ya wapinzani wao wa karibu Borussia Dortmund, ingawa wamecheza mchezo mmoja zaidi.

Augsburg, ambao  hawakuwa wameshinda katika michezo yao mitano iliyopita, wanapanda hadi nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi, wakiwa na tofauti ya pointi nne juu ya eneo la mchujo wa kushuka daraja.