Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern yakaribia kumaliza kazi dili la Anthony Gordon

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Gordon ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Newcastle kiasi cha kuivutia sana Bayern ambayo ilianza kuonyesha nia ya kumsajili dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

BAYERN Munich wamefikia makubaliano binafsi, Anthony Gordon, 25, na sasa wameanza mazungumzo na rasmi na Newcastle United kujua ada ya uhamisho inayohitajika ili kuipata saini ya staa huyo.

Gordon ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Newcastle kiasi cha kuivutia sana Bayern ambayo ilianza kuonyesha nia ya kumsajili dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Mkataba wa Gordon unatarajiwa kumalizika mwaka 2030 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 46 za michuano yote na kufunga mabao 17.

Licha ya kuwa imefika makubaliano na upande wa mchezaji, dili la Gordon kutua Bayern bado linaonekana kuwa na ugumu sana kutokana na pesa ambazo Newcastle inazihitaji ili kumuuza.

Kwa mujibu wa ripoti za awali, Gordon ambaye msimu huu pia ametoa asisi tano, alikuwa anauzwa kwa takribani Euro 100 milioni, kiasi ambacho Bayern haionekani kuwa tayari kukitoa.

Hata hivyo, kwa sasa haijajulikana ikiwa Newcastle itaendelea kushikilia msimamo wa kutaka kiasi hicho cha pesa au itakubali kukishusha.


Ander Barrenetxea

CHELSEA na Manchester United zimemweka mshambuliaji wa Real Sociedad na Hispania, Ander Barrenetxea, 24, kwenye orodha yao ya wachezaji inaotaka kuwasajili katia dirisha la majira haya ya kiangazi.

Vigogo hawa wawili wanapambana kuhakikisha wanaboresha safu zao za ushambuliaji na Barrenetxea anaonekana kuwa mtu sahihi kwao.

Hata hivyo, hadi sasa haijajulikana ikiwa Sociedad itakuwa tayari kumwachia fundi huyo mwisho wa msimu huu, ingawa taarifa za ndani ziandai dili lolote la staa huyu kuuzwa huenda likagharimu zaidi ya Pauni 60 milioni.


Elliot Anderson

MANCHESTER United ipo katika mchakato wa kutuma rasmi ofa kwenda Nottingham Forest kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu hiyo na England, Elliot Anderson, 23, ili kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Anderson amekuwa akihitaji na vigogo wa Ulaya kwa muda mrefu lakini mara zote, Forest imekuwa ikigoma kumuuza na kusisitiza kwamba bado wana mipango naye.

Mkataba wa sasa wa Anderson unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na msimu huu amecheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao manne.


Jonathan Rowe

CHELSEA na Galatasaray zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Bologna na England, Jonathan Rowe, 23, dirisha lijalo.

Rowe ameanza kuvutia macho ya klabu mbalimbali barani Ulaya kwa muda sasa, lakini hakuna hata moja iliyowahi kuwasilisha ofa rasmi hapo awali.

Kwa sasa Chelsea ndio inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumpata kwani mchezaji mwenyewe ameonyesha kuvutiwa zaidi na ofa yao badala ya Galatasaray kwani anaamini soka la England la England lina ushindani zaidi tofauti na ilivyo Uturuki.


Nick Woltemade

STAA wa Newcastle United, Nick Woltemade ameripotiwa kutokuwa na furaha ndani ya kikosi hicho na huenda akakubali ofa ya kujiunga na Atletico Madrid ili kupata changamoto mpya.

Mshambuliaji huyo wa Ujerumani, 24, anatajwa kuwa chini ya uangalizi wa vilabu kadhaa kutokana na kutoridhishwa kwake na nafasi ya kucheza.

Kwa upande wa Newcastle, hali hiyo inaweza kuwalazimu kufanya maamuzi ya haraka kuhusu mustakabali wake ili kuepuka kupoteza mchezaji bila mpango.

Iwapo ataondoka, huenda Woltemade akawa mmoja wa majina mapya katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.


Mason Greenwood

MSHAMBULIAJI wa Marseille, Mason Greenwood, 24, anatarajiwa kubaki katika timu hiyo licha ya kuhusishwa na klabu kubwa Ulaya kama Juventus, Borussia Dortmund na Atlético de Madrid.

Ripoti zinaeleza Greenwood amepanga kuendelea na maisha yake ya soka Ufaransa kutokana na utulivu wa nafsi yake pia umuhimu katika klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa England alidaiwa huenda angerejea EPL kuungana na kocha Roberto de Zerbi katika kikosi cha Tottenham.


Benjamin Pavard

MARSEILLE haina mpango wa kutumia kipengele cha kumnunua mazima beki wa kimataifa wa Ufaransa, Benjamin Pavard, 30, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu yao akitokea Inter Milan, kwa sababu hawajaridhishwa na kiwango chake licha ya kumtumia.

Beki huyo wa zamani wa Bayern Munich ni miongoni mwa  mchezaji wenye uzoefu mkubwa na soka la Ulaya, lakini kiwango chake katika miaka ya hivi karibuni hakiridhishi.

Pavard aliwika sana akiwa na Ufaransa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 akiwa na Ufaransa iliyochukua ubingwa.


Yan Diomande

CHELSEA na Liverpool zimehusishwa na winga wa Ivory Coast, Yan Diomande, 19, ambaye anachezea RB Leipzig.

Ripoti zinaeleza mchezaji huyo kijana anaweza kugharimu takribani Pauni  80 milioni kama ada ya uhamisho. Hata hivyo, hadi kufikia sasa,

Diomande mwenyewe hajaweka wazi ikiwa atakuwa tayari kuondoka au laa ingawa inaaminika ikitokea timu inayomhitaji itamalizana na Leipzig yeye hana kipingamizi chochote.