Barca kumshtaki De Jong

CATALUNYA, HISPANIA. KLABU ya Barcelona itamfungulia mashtaka Frankie de Jong, kutokana na makosa ya yaliyojitokeza kwenye mkataba wake wa awali.
Miamba hiyo itaanza taratibu za kisheria ili kuutazama upya uhalali wa mkataba huyo kwa mujibu wa ripoti.
Imeelezwa Barcelona ilipiatia mkataba wa De Jong na kugundua kuna maghumashi, huku ikimuonya  kiungo huyo anayewindwa Man United dirisha hili.
Mpaka sasa haijafahamika endapo De Jong atabaki Camp Nou kwani Man United na Barcelona, zilifikia makubaliano ya ada yake ya Uhamisho Euro 85 milioni, ambayo italipwa kwa awamu.