Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la McTominay lawekwa kwenye noti Scotland

Muktasari:

  • Kiungo Scott McTominay amepewa heshima ya kipekee baada ya Benki ya Scotland kuzindua noti maalum ya pauni 20 yenye picha ya bao lake la kubinuka (overhead kick) dhidi ya Denmark, lililochochea Scotland kufuzu Kombe la Dunia 2026 katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Denmark.

ILI kuadhimisha kurejea kwa Scotland kushiriki Fainali za Kombe la Dunia ikipita takribani miaka 28, moja kati ya bao la kuvutia lililofungwa hivi karibuni katika historia ya taifa hilo, sasa linaenziwa hadi kwenye noti za fedha.

Kiungo Scott McTominay amepewa heshima ya kipekee baada ya Benki ya Scotland kuzindua noti maalum ya pauni 20 yenye picha ya bao lake la kubinuka (overhead kick) dhidi ya Denmark, lililochochea Scotland kufuzu Kombe la Dunia 2026 katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Denmark.

Mechi hiyo ya mwisho kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyochezwa Novemba 18, 2025, McTominay alifunga bao hilo dakika ya pili ambapo ushindi huo uliifanya Scotland kuongoza kundi C na kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Noti hizo maalum ni 100 pekee zilizochapishwa. Kati yake, 50 zitapatikana kupitia mnada wa wakusanyaji, droo ya zawadi, pamoja na “vaults” mbili za muda zitakazowekwa katika miji ya Glasgow na Edinburgh. Sehemu ya mapato yatasaidia Crisis Scotland, shirika la kusaidia watu wasio na makazi.

McTominay, ambaye anacheza kiungo kwa timu ya taifa ya Scotland na klabu ya Napoli ya Italia, amesema: “Nyakati kama hizo ni za kila mtu anayeliunga mkono taifa letu. Kwa hiyo kuona bao langu likiwekwa kwenye noti ya Scotland ni jambo maalum sana.”

Emma Noble, mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya Scotland katika benk ya nchi hiyo, amesema walitaka kuadhimisha kufuzu kwa timu hiyo kwa njia inayowakilisha utambulisho wa Kiscotland.

Amesema: “Kama ilivyo kwa soka, noti za fedha zimekuwa sehemu ya historia ya nchi yetu kwa muda mrefu. Noti hii maalum ya pauni 20 inaunganisha tamaduni hizo mbili kwa mtindo wa kisasa na wa ubunifu.”

Mara ya mwisho Scotland ilishiriki Kombe la Dunia mwaka 1998. Katika mashindano ya mwaka huu yatakayofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11, Scotland imepangwa kundi C na Haiti, Morocco na Brazil.