Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bale aogopa kufilisika

Muktasari:

  • Staa wa zamani wa Tottenham Hotspur na Real Madrid, Bale, 36, alitundika daruga zake kwenye soka baada ya fainali za Kombe la Dunia 2022.

CARDIFF, WALES: SUPASTAA, Gareth Bale amefichua jambo linalompa hofu kubwa kuwa ni kufilisika.

Staa wa zamani wa Tottenham Hotspur na Real Madrid, Bale, 36, alitundika daruga zake kwenye soka baada ya fainali za Kombe la Dunia 2022.

Bale kuna wakati alikuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwenye soka wakati aliposaini mkataba wa miaka sita uliokuwa na thamani ya Pauni 150 milioni huko Real Madrid mwaka 2016.

Kuna ripoti zinafichua Bale aliwahi kuripotiwa kuwa na kipato cha Pauni 120 milioni.

Licha ya kuvuna pesa nyingi, Bale mara zote amekuwa makini kwenye matumizi.

Staa huyo wa Wales ana watoto watatu aliozaa na mkewe, mrembo Emma Rhys-Jones na alisema: “Kuna kitu kimoja ambacho mara zote kimekuwa kikinitisha sana. Siku zote unasoma habari za kwamba kuna watu walipomaliza tu soka la kulipwa, wamefilisika.

“Hawakujua namna ya kuhitaji pesa zao, hawana uelewa wa jambo hilo. Kuna vitu vingi sana, wachezaji wanapenda maisha ya starehe. Najaribu kujiepusha na hilo. Mimi nilifahamu mapema, nitakapoacha soka sitakuwa na malipo tena.”

Bale alisema alipenda sana kuhamia kwenye soka la Ligi Kuu Marekani kabla ya kupata kipindi kifupi huko LAFC, lakini mshahara umekuwa tatizo.

Tangu alipostaafu soka, Bale amekuwa akifanya shughuli za uchambuzi wa soka TNT Sports, ikiwamo kuchambua kwenye mechi ya fainali ya Europa League mwaka jana.