Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bado mechi mbili tu

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia

Muktasari:

Wakati John Terry akiongoza wachezaji wa Chelsea kushangilia juzi mara baada ya mechi, Mourinho amewataka wachezaji wake wanyamaze na wasishangilie kabisa mpaka wakishinda mechi mbili zijazo

BADO mechi mbili tu. Mbili tu siyo zaidi. Ndicho anachoamini Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho baada ya juzi usiku kuichapa Manchester United 1-0 katika dimba la Stamford Bridge.

Wakati John Terry akiongoza wachezaji wa Chelsea kushangilia juzi mara baada ya mechi, Mourinho amewataka wachezaji wake wanyamaze na wasishangilie kabisa mpaka wakishinda mechi mbili zijazo.

Chelsea itakuwa katika Jiji la London wikiendi ijayo kucheza dhidi ya Arsenal ugenini kabla ya kucheza na Leicester City ambayo inapigana isishuke daraja. Mourinho amewataka wachezaji wake waache kushangilia kwa sasa.

“Katika soka bado. Ni suala la hesabu. Tutakapokamilisha hesabu kazi itakuwa imekwisha. Tutashangilia. Mpaka wakati huo tunahitaji kushinda mechi mbili kuwa mabingwa. Inabidi tushinde mechi,” alisema Mourinho.

“Tunaweza kusema tutapata pointi tisa nyumbani. Tunaweza kuwa mabingwa tukiwa nyumbani kwa kucheza mechi zetu za nyumbani. Kama tukipata pointi ugenini itakuwa bora pia,” alisema Mourinho.

Kocha huyo alikipongeza kikosi chake kilichocheza juzi dhidi ya Manchester United ambacho kilipata ushindi wake kupitia bao la staa wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard aliyefunga bao murua la tobo akikokota mpira alioupokea kutoka kwa Oscar.

“Timu ilikuwa bora sana. Mimi ndiye ninayejua jinsi gani ilikuwa bora. Mechi ilikwenda kama nilivyotaka. Tunapohitaji kucheza mechi huwa tunacheza mechi. Mechi ilikuwa nzuri,” alijigamba Mourinho.

“Eden ana yale maajabu ambayo wachezaji wakubwa wanakuwa nayo, sana sana katika mechi kubwa. Ulikuwa ni msingi mkubwa sana kwetu. Nadhani (Gary) alifanya kazi kubwa kuzuia shuti la Falcao. John Terry alikuwa bora sana. kipa alifanya vizuri pia.”

“(Cesar) Azpilicueta kwangu mimi alikuwa mchezaji bora uwanjani. (Nemanja) Matic alifanya kazi kama mnyama. (Kurt) Zouma alimtoa (Marouane) Fellaini nje ya mchezo. Namba 11 (Didier Drogba) alikuwa mnyama mwingine uwanjani.”

“Oscar alifanya kazi nzuri, Ramires alikuja na kufanya tulichotaka. Hata John Obi Mikel alikuja na kukaa na mpira vizuri. Na Willian ambaye alikuwa amelala kitandani kwa siku mbili aliondoka nyumbani na kuja kutupa kidogo alichokuwa nacho.”

Kwa sasa Chelsea inaongoza kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya Arsenal ikiwa na pointi 76 huku Arsenal ikiwa na pointi 66. Matokeo hayo yameiacha Manchester United ikibakiwa na pointi 65 mkononi.