Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta na safari yake ya matumaini leo

Muktasari:

  • Mchezo huo utakoanza saa 12:30 utakuwa wa kujiuliza kwa Arteta ambaye anapata shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wengi wanataka aondoke wakiamini ameshindwa kuifanya timu hiyo ichukue ubingwa wa EPL jambo ambalo wanalihitaji kwa muda mrefu.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England inaendelea leo na mchezo ambao unatarajiwa kuvutia mashabiki wengi zaidi ni ule wa Newcastle United itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Arsenal ya Mikel Arteta.

Mchezo huo utakoanza saa 12:30 utakuwa wa kujiuliza kwa Arteta ambaye anapata shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wengi wanataka aondoke wakiamini ameshindwa kuifanya timu hiyo ichukue ubingwa wa EPL jambo ambalo wanalihitaji kwa muda mrefu.

Hadi kufikia jana jioni washika mitutu hao wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England na mechi hii inahitaji sana kushinda ili kutoweka utofauti mkubwa wa alama kati yao na vinara Liverpool ambayo kabla ya mechi yake ya jana dhidi ya Manchester City ilikuwa ni pointi tano.

Rekodi zinaonyesha Arsenal haina matokeo mazuri mbele ya Newcastle hivi karibuni kwani katika mechi nne za mwisho za michuano yote, imepoteza tatu na kushinda moja.

Arteta anahitaji zaidi mchezo huu kwa ajili ya kuendelea kushindana katika mbio za ubingwa na kutoachwa kwa alama nyingi kwani mashabiki wanahitaji kuona akishinda taji.

Mbali ya mechi hii, kesho Aston Villa ambayo imekuwa katika wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Villa Park kuikaribisha Fulham.

Kwa sasa Villa ambayo inanolewa na kocha Unai Emery inashika nafasi ya 18 ikiwa na pointi tatu tu ilizokusanya baada ya kutoa sare tatu na kufungwa mechi mbili kati ya tano za msimu huu.

Itaenda kukutana na Fulham ambayo imeanza msimu vizuri ikiwa inashika nafasi ya nane baada ya kushinda mechi mbili, sare mbili na kufungwa moja tangu kuanza kwa msimu.

Mechi hii inatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni na kesho pia kutakuwa na mechi moja kwenye Monday Night Football ambapo Everton ikiwa kwenye uwanja wake wa Goodson Park itaikaribisha West Ham iliyoachana na kocha wake Graham Potter jana.

West Ham ilimfungashia virago kocha huyo wa zamani wa Brighton na Chelsea baada ya kiwango kibovu kilichoonyeshwa na timu yao tangu achukue mikoba ya kuinoa Januari mwaka huu.

Msimu huu katika mechi tano West Ham imekusanya alama tatu tu baada ya kushinda mechi moja na kupoteza nne huku ikishika nafasi ya 10