Arteta: Majeruhi? Wote wapo fiti
Muktasari:
- Kocha huyo Mhispaniola anaamini Kai Havertz ambaye alikosa mechi ya kipigo cha mabao 3-2 kutoa kwa Villarreal uwanjani Emirates, Jumatano iliyopita inaamini atarejea uwanjani kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Athletic Bilbao wikiendi hii.
LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kwamba atamaliza tatizo la majeruhi kabla ya msimu kuanza.
Kocha huyo Mhispaniola anaamini Kai Havertz ambaye alikosa mechi ya kipigo cha mabao 3-2 kutoa kwa Villarreal uwanjani Emirates, Jumatano iliyopita inaamini atarejea uwanjani kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Athletic Bilbao wikiendi hii.
Leandro Trossard na Riccardo Calafiori nao walikosa mechi hiyo ya Emirates, lakini inaaminika watakuwapo kwenye mechi ya mwisho ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England, ambapo mechi ya kwanza watakipiga na Manchester United, Agosti 17.
Mchezaji pekee ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu ni straika Gabriel Jesus, ambaye hajacheza tangu Januari.
Alipoulizwa kuhusu Havertz, Arteta alisema: “Jana kwenye mazoezi alihisi kitu na asubuhi hakujisikia vizuri, hivyo tumeamua kumpumzisha.
“Nadhani atakwenda kuwa fiti ndani ya siku chache, matumaini atarejea wikiendi, kama kila kitu kitakwenda sawa, nadhani atakuwa fiti.”