Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta ataja sababu kuukosa ubingwa EPL

Muktasari:

  • Arsenal inatarajiwa kumaliza ndani ya nne bora, lakini ikiwa ni mara ya tatu ikiukosa ubingwa baada ya kuanza vyema msimu, huku uliopita ikimaliza ikiwa ya pili nyuma ya Manchester City iliyobeba ubingwa ikiwa na pointi 91 ikiwa ni mbili mbele ya Washika Mitutu hao waliomaliza na 89.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amedokeza kuwa majeraha na kadi walizokutana nazo msimu huu ni sababu ya timu hiyo kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Arsenal inatarajiwa kumaliza ndani ya nne bora, lakini ikiwa ni mara ya tatu ikiukosa ubingwa baada ya kuanza vyema msimu, huku uliopita ikimaliza ikiwa ya pili nyuma ya Manchester City iliyobeba ubingwa ikiwa na pointi 91 ikiwa ni mbili mbele ya Washika Mitutu hao waliomaliza na 89.

Timu hiyo pia iliukosa ubingwa wa mashindano hayo msimu wa 2022-23 nyuma ya Man City iliyomaliza na pointi 89 ilhali yenyewe ikimaliza na 84.

Hata hivyo, Arteta amesema msimu huu ulikuwa wao kubeba ubingwa, lakini wameangushwa na majeraha ya mara kwa mara kwa wachezaji muhimu huku pia kadi walizokutana nazo mchezoni zikichangia.

Alisema majeraha na kadi vimekuwa vikwazo kwa timu yake katika harakati za kutwaa ubingwa, jambo ambalo linawaumiza wote.

Iwapo Arsenal watapoteza dhidi ya Ipswich Town leo, Jumapili katika mechi ya ligi na Liverpool kuwafunga Leicester City, basi vijana wa Arne Slot watajihakikishia ubingwa.

Msimu huu, The Gunners wamekumbwa na matatizo kadhaa ikiwa ni pamoja na majeraha kwa wachezaji muhimu kama Bukayo Saka, Martin Odegaard na Kai Havertz, sambamba na uamuzi tata wa waamuzi. Matukio hayo ni pamoja na kadi nyekundu ya Myles Lewis-Skelly dhidi ya Wolves aliyoipata Januari  ambayo baadaye ilifutwa na FA baada ya rufaa pamoja na kadi nyekundu aliyopewa Declan Rice kwa kucheza mpira baada ya filimbi dhidi ya Brighton Agosti, mwaka jana.

Alipoulizwa kama Arsenal wangeweza kufanya zaidi kuhimili ushindani wa Liverpool, Arteta alisema: “Kwa hakika kuna mambo ambayo tungeweza kufanya... tungeshinda kila mchezo bila kujali majeraha na kadi zisingekuandama..”