Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta achekea sub zake Arsenal

Muktasari:

  • Arteta mabadiliko yake ya wachezaji ndiyo yaliyoleta tofauti kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ikifunga mara mbili na wachezaji wa kutokea benchi kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kwa msisitizo kwamba Gabriel Martinelli  na Leandro Trossard watalazimika kuzoea maisha ya kuanzia benchini na kuingia uwanjani kama “super subs” kuliko kuanza kwenye mechi za miamba hiyo ya Emirates.

Arteta mabadiliko yake ya wachezaji ndiyo yaliyoleta tofauti kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ikifunga mara mbili na wachezaji wa kutokea benchi kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao.

Arsenal haikuwa kwenye ubora wake katika mechi hiyo ya Basque Country, ambapo straika wao Viktor Gyokeres alikosa nafasi kadhaa za kufunga, huku Eberechi Eze akishindwa kuonyesha ubora mkubwa kwenye wingi ya kushoto. Usiku wa mechi hiyo ulikuwa na presha kubwa hadi hapo Martinelli na Trossard walipoingizwa kutokea benchini na kuokoa jahazi.

Trossard alimtengenezea nafasi Martinelli kufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-0 baada ya umaliziaji mzuri, kabla ya staa huyo wa Kibrazili naye kulipa fadhila kwa mtu aliyempikia bao la kwanza. Arteta alivutiwa na mchango uliofanywa na wachezaji wake waliotokea benchini na kuwaambia kitu baada ya mechi hiyo kumalizia.

“Safi sana kwao, kwa Martinelli na Leo. Walikuwa na viwango tofauti kabisa na Ebs na Viktor,” alisema kocha huyo wa Emirates na kuongeza. “Niliwaingiza na baada ya muda tu wakaanza kuonyesha muunganiko wao mzuri. “Nimefarijika kwa sababu niliwaambia: ‘Jamani, muda wote mmekuwa muhimu, hivyo onyesheni ubora wenu kwenye dakika hizi muhimu’. Na nimefurahi kwa sababu wametusaidia sana.”