Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaingia hasara kuruhusu wachezaji kusepa

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa michezo wa kikosi hicho cha Emirates, Andrea Berta alikuwa bize kuwafungulia mlango wa kutokea mastaa ambao hawakuwa kwenye mipango yao ili kuweka sawa vitabu vya hesabu za fedha.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imeripotiwa kuingia hasara ya kuruhusu wachezaji wenye kipaji chenye thamani ya Pauni 47 milioni kuondoka kwenye timu kwa Pauni 260,000 tu kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Mkurugenzi wa michezo wa kikosi hicho cha Emirates, Andrea Berta alikuwa bize kuwafungulia mlango wa kutokea mastaa ambao hawakuwa kwenye mipango yao ili kuweka sawa vitabu vya hesabu za fedha.

Arsenal ilitumia zaidi ya Pauni 250 milioni kunasa wachezaji wapya kwenye dirisha la majira ya kiangazi, hivyo ilihitaji kuwaruhusu wengine kuondoka ili kukifanya kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kuwa kwenye uwiano mzuri.

Viktor Gyokeres, Martin Zubimendi, Noni Madueke, Cristhian Mosquera, Christian Norgaard, Eberechi Eze, Kepa Arrizabalaga na Piero Hincapie walitua kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Arteta. Na baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo wa Hincapie kutoka Bayer Leverkusen, Berta sasa alihamishia mawazo kwenye orodha ya wachezaji wanaopaswa kuondoka.

Arsenal ilikamilisha dili sita za kuwafungulia mlango wa kutokea wachezaji wake kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili, Septemba 1, ilipowapa mkono wa kwa heri Oleksandr Zinchenko, aliyejiunga kwa mkopo Nottingham Forest, Jakub Kiwior, aliyetimkia Porto, Reiss Nelson, aliyeenda kwa mkopo Brentford, na Lucas Nygaard, ambaye alienda kujiunga Brabrand kwa mkopo. Ilifanya dili mbili pia na klabu ya Hamburg, ilipowapeleka viungo Fabio Vieira na Albert Sambi Lokonga kwenye klabu hiyo ya Ujerumani.

Vieira alijiunga na Arsenal kutokea Porto kwa ada ya Pauni 30 milioni mwaka 2022, lakini ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha Arteta. Kiungo huyo mchezeshaji amefunga mabao matatu na asisti 10 katika mechi 49 alizochezea Arsenal, lakini sasa amejiunga na Hamburg kwa mkopo wa msimu mzima baada ya kutumika kwa mkopo pia huko Porto msimu uliopita.

Sambi Lokonga alijiunga na Anderlecht mwaka 2021 kwa ada ya Pauni 17 milioni na baada ya mkopo Crystal Palace, Luton na Sevilla, ameondoka Arsenal jumla kwenda Hamburg. Kiungo huyo aliyechezea Arsenal mara 39 bila ya kufunga wala kuasisti, ameuzwa kwa Pauni 260,000 tu. Lakini, kama Hamburg haitashuka daraja, basi italazimika kuilipa Arsenal ada ya Pauni 17 milioni kwa ajili ya huduma ya staa huyo.