Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal walia ratiba yao kimeo

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Emirates imefahamu namna itakavyoanza kwa mechi kali kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England baada ya ratiba ya mikikimikiki hiyo kutolewa rasmi Jumatano asubuhi.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Arsenal wametania kwamba ratiba ya mechi zao sita za kwanza kwenye Ligi Kuu England msimu ujao ni ya “hujuma”.

Miamba hiyo ya Emirates imefahamu namna itakavyoanza kwa mechi kali kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England baada ya ratiba ya mikikimikiki hiyo kutolewa rasmi Jumatano asubuhi.

Na jeshi hilo la kocha Mikel Arteta lilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa misimu mitatu mfululizo, imeona kasheshe la msimu ujao litakavyokuwa baada ya ratiba kutoka.

Wababe hao wa London Kaskazini wataanza kampeni yao Agosti 17 kwa mechi ya ugenini huko Old Trafford kukabiliana na Manchester United, ambao bila shaka watakuwa na nyota wengi wapya kikosini kwao.

Baada ya hapo itarudi Emirates kucheza na Leeds United wikiendi inayofuatia kabla ya kwenda Anfield kukabuliana na mabingwa watetezi Liverpool katika ratiba yao ya Agosti 30.

Kisha Arsenal itarudi nyumbani kucheza na Nottingham Forest uwanjani Emirates, Septemba 13 ikifuatia mapumziko ya mechi za kimataifa. Arsenal itahitimisha mwezi kwa mechi za kibabe, itakapokabiliana na Manchester City ya Pep Guardiola uwanjani Emirates na kisha kwenda St James’ Park kuwakabili mabingwa wa Kombe la Ligi, Newcastle United.

Jambo hilo limewaibua mashabiki wa Arsenal na kutania kwamba hiyo ratiba itakuwa ni ya ‘kuwahujumu’, licha ya kwamba ni kompyuta ndiyo iliyofanya mchakato wote.

Shabiki mmoja aliandika kwenye X: “Hii ligi ni kama inataka kututengeneza hivi.”

Mwingine alisema: “Hii ligi imepangwa.”

Na shabiki mwingine aliongeza: “Ile ratiba ni ya mchongo kabisa.”

Kuna shabiki alisema: “Asitokee mtu kuniambia hii ratiba sio hujuma.”

Na kuna shabiki kwa hasira alisema neno moja tu: “Imepangwa.”

Hata hivyo, hakuna bosi yeyote wa Arsenal aliyelalamikia kuwa ratiba hiyo ni ya kuwahujumu. Arsenal inaonekana kuwa na mwanzo mgumu, mambo yao yatakuwa mepesi mwishoni mwa msimu ambapo itakuwa na mechi za kukabiliana  na Fulham, West Ham, Burnley na Crystal Palace katika mechi zao mwisho za mwisho.