Arsenal bana, eti waamini jezi itashinda
Muktasari:
- Arsenal itakwenda Old Trafford kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Jumapili.
LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Arsenal wanaamini timu yao itaichapa Manchester United kwenye mchezo wao wa kwanza baada ya kubainisha jezi ambazo zitavaliwa na mastaa katika mechi hiyo ya Old Trafford.
Arsenal itakwenda Old Trafford kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Jumapili.
Mechi hiyo itakuwa msingi mzuri kwa Arsenal katika haraka zao za kuanza msimu vizuri endapo kama itafanikiwa kuichapa Man United.
Chama hilo la Kocha Mikel Arteta lilimaliza nafasi ya pili kwenye ligi msimu uliopita na ilikuwa mara ya tatu mfululizo.
Sasa mashabiki wa miamba hiyo ya Emirates wanaamini wataondoka kwenye Jiji la Manchester wakiwa na pointi zote tatu. Hii ni kwa sababu itavaa jezi yao mpya namba tatu katika mechi hiyo. Jezi hiyo inafanana kabisa na ile iliyotumiwa na timu hiyo kwenye msimu wa 2007/08.
Shabiki mmoja alisema: “Tunawataka wavae jezi zao bora hatutaki kisingizio.”
Shabiki wa pili alisema: “Jezi hii italeta kumbukumbu bora msimu huu.”
Na shabiki wa tatu alisema: “Hii jezi inatupa mzuka wa kushinda.”
Shabiki wa nne alisema: “Hatuwezi kupoteza mechi kwenye jezi nzuri hivyo.”
Mwingine aliongeza: “Tunakwenda kule kuwapika Man United.”
Msimu uliopita, Arsenal ilinusurika kipigo Old Trafford kwenye mchezo wa Ligi Kuu England shukrani kwa bao la Declan Rice, kufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1, wakati bao la Man United lilifungwa kwa mkwaju wa adhabu na kiungo mshambuliaji, Bruno Fernandes.
Arsenal itakwenda kwenye mechi hiyo ikitokea kucheza mechi tano za pre-season na ilishinda tatu na kupoteza mbili. Walizichapa AC Milan, Newcastle na Athletic Bilbao na ilichapwa na Tottenham na Villarreal.
Mechi hiyo itashuhudia sura mpya kadhaa za Arsenal ikiwamo Martin Zubimendi, Victor Gyokeres, Noni Madueke, Christian Norgaard na Cristhian Mosquera.