Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arne Slot presha ipo juu kisa mastaa wake

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa shoka alilazimika kufanyiwa mabadiliko kipindi cha pili, wakati wa mchezo wa ushindi wa mabao 3-0 wa Argentina dhidi ya Chile.

LIVERPOOL, ENGLAND: KIJASHO kinamtoka Kocha wa Liverpool, Arne Slot baada ya kiungo wake Alexis Mac Allister kupatwa na maumivu ya misuli wakati alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Argentina Alhamisi iliyopita.

Kiungo huyo wa shoka alilazimika kufanyiwa mabadiliko kipindi cha pili, wakati wa mchezo wa ushindi wa mabao 3-0 wa Argentina dhidi ya Chile.

Mac Allister, 25, aling’ara kwenye kiungo Jumapili iliyopita wakati Liverpool ilipoichapa Manchester United uwanjani Old Trafford na sasa amempa presha kocha wake kwa kushindwa kumaliza mechi hiyo ya kimataifa alipotolewa dakika ya 79 kutokana na kuwa na maumivu kwenye mguu wa kulia.

Mac Allister alipatiwa matibabu kutokana na tatizo hilo kabla ya kutolewa uwanjani huko kocha wa Argentina, Lionel Scaloni akishindwa kuweka wazi kiungo huyo wa Colombia kama atakuwa fiti kutumika kwenye mchezo ujao, Jumanne dhidi ya Colombia.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ushindi huo, ambapo Mac Allister alifunga bao la kwanza, alisema: “Bado hatufahamu ni muda gani Mac Allister na Nicolas Gonzalez watakuwa nje kutokana na kuumia na kama watakuwa fiti kucheza mechi ijayo, bado mapema.”

Wasiwasi wa kocha Slot unazidi baada ya kiungo mwingine wa Liverpool, Harvey Elliott kuondoshwa kwenye kikosi cha England cha U21 kutokana na kuwa majeruhi.

Liverpool itarejea uwanjani Septemba 14 kukabiliana na Nottingham Forest mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Uwanja wa Anfield. Baada ya mechi hiyo, kikosi hicho cha Slot kitakuwa na kasheshe la kuikabili AC Milan kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kukipiga na Bournemouth na West Ham United kwenye raundi ya tatu ya Kombe la Ligi.

Badaaye watakipiga na Wolves, Bologna na Crystal Palace kabla ya mapumziko mengine ya mechi za kimataifa, Oktoba.