Argentina yatangaza 55 kikosi cha awali
Muktasari:
- Kocha Lionel Scaloni amefanya uamuzi kadhaa mkubwa huku mastaa sita waliokuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar wakikosekana. Wachezaji hao ni Franco Armani, Juan Foyth, Angel Di Maria, Angel Correa, Papu Gomez na Paulo Dybala.
BUENOS AIRES, ARGENTINA: MABINGWA watetezi wa Kombe la Dunia, Argentina, wameanza rasmi maandalizi ya kutetea taji kwa kutangaza kikosi cha awali cha wachezaji 55 kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu.
Kocha Lionel Scaloni amefanya uamuzi kadhaa mkubwa huku mastaa sita waliokuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar wakikosekana. Wachezaji hao ni Franco Armani, Juan Foyth, Angel Di Maria, Angel Correa, Papu Gomez na Paulo Dybala.
Kwa upande mwingine, jina la Gianluca Prestianni limekuwa mshangao mkubwa licha ya kwamba mchezaji huyo wa Benfica atakosa mechi mbili za mwanzo kutokana na adhabu ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), kuhusiana na sakata la ubaguzi dhidi ya Vinicius Jr lililotokea wakati wa mechi ya kuwania kufuzu nusu fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Benfica na real Madrid.
Scaloni ameendelea kuwaamini mastaa wake wakubwa akiwemo Lionel Messi ambaye anatarajiwa kucheza Kombe lake la mwisho la Dunia.
Wachezaji wengine waliopo kwenye kikosi hicho ni Emiliano Martinez, Cristian Romero, Rodrigo De Paul, Enzo Fernandez, Alexis Mac Allister na Lautaro Martinez. Kinda Franco Mastantuono wa Real Madrid naye amejumuishwa kwenye kikosi hicho, jambo linaloonyesha jinsi Argentina inavyoanza kuandaa kizazi kijacho cha timu hiyo.
Kikosi kamili kinawajumuisha Emiliano Martinez (Aston Villa), Geronimo Rulli (Marseille), Juan Musso (Atletico Madrid), Walter Benitez (Crystal Palace), Facundo Cambeses (Racing Club), Santiago Beltran (River Plate), Agustin Giay (Palmeiras), Gonzalo Montiel (River Plate), Nahuel Molina (Atletico Madrid), Nicolas Capaldo (Hamburg SV) na Kevin Mac Allister (Union St Gilloise).
Wengine ni Lucas Martinez (River Plate), Marcos Senesi (Bournemouth), Lisandro Martínez (Manchester United), Nicolas Otamendi (Benfica), German Pezzella (River Plate), Leonardo Balerdi (Marseille), Cristian Romero (Spurs), Lautaro Di Lollo (Boca Juniors), Zaid Romero (Getafe), Facundo Medina (Marseille), Marcos Acuna (River Plate) na Nicolas Tagliafico (Lyon).
Pia kuna Gabriel Rojas (Racing Club), Maximo Perrone (Como), Lleandro Paredes (Boca Juniors), Guido Rodriguez (Valencia), Aníbal Moreno (River Plate), Milton Delgado (Boca Juniors), Alan Varela (FC Porto), Ezequiel Fernandez (Leverkusen), Rodrigo De Paul (Inter Miami), Exequiel Palacios (Leverkusen), Enzo Fernandez (Chelsea), Alexis Mac Allister (Liverpool), Giovani Lo Celso (Real Betis Balompie) na Nicolas Dominguez (Nottingham Forest).
Nyota wengine ni Emiliano Buendia (Aston Villa), Valentín Barco (RC Strasbourg), Lionel Messi (Inter Miami), Nicolas Paz (Como), Franco Mastantuono (Real Madrid), Thiago Almada (Atletico Madrid), Tomas Aranda (Boca Juniors), Nicolas Gonzalez (Atletico Madrid), Alejandro Garnacho (Chelsea), Giuliano Simeone (Atletico Madrid), Matias Soule (AS Roma), Claudio Echeverri (Girona), Gianluca Prestianni (Benfica), Santiago Castro (Bologna), Lautaro Martinez (Inter Milan) na Jose Manuel Lopez (Palmeiras)