Antony apigwa 'stop'

MANCHESTER, ENGLAND. WINGA wa Manchester United, Anthony hatarejea kwenye kikosi hadi uchunguzi wa polisi utakapokamilika taarifa rasmi imetolewa na klabu hiyo.

Winga huyo ameshtakiwa kwa makosa ya kumpiga na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani Gabiela Cavallin sasa amepewa muda zaidi wa kushirikiana na polisi.

Chanzo cha habari kimeripoti ishu hiyo imekuwa ‘siriazi’ huku uongozi wa klabu ukiendelea kufuatilia kesi hiyo kwa kina.

Kufuatia majadiliano kati ya mtendaji wa klabu hiyo Richard Arnold na kocha wake Erik ten Hag uongozi umeamua kumuondoa kikosi baada ya timu ya taifa ya Brazil kumtema.

"Tunafahamu tuhuma zinazomkabili Antony, wachezaji ambao hawajacheza mechi za kirafiki wanatakiwa kurudi leo, lakini tumefia makubaliano kwamba Antony hatarejea hadi uchunguzi utakapokamilika. Kama klabu tunakemea matendo maovu,"

Antony bado hajakamatwa lakini polisi wameendelea na uchunguzi kufuatia shutma hizo dhidi yake kwa mujibu wa taarifa.

Nyota huyo wa zamani wa Ajax alikana tuhuma hizo kupitia kituo cha televisheni cha Brazil akisisitiza kwamba ni hatia ukweli utajulikana.