Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anthony Gordon mambo safi Barcelona

GORDON Pict

Muktasari:

  • Winga huyo aliondoka Newcastle International Airport majira ya saa 5:10 asubuhi kwa saa za England kabla ya kutua Hispania kwa ajili ya vipimo vya afya akitarajiwa kukamilisha dili lake kesho.

BARCELONA, HISPANIA: NYOTA wa England na Newcastle United, Anthony Gordon, amewasili jijini Barcelona kwa ndege binafsi kukamilisha dili lake la pauni 70 milioni kwenda kwa mabingwa hao wa Hispania.

Winga huyo aliondoka Newcastle International Airport majira ya saa 5:10 asubuhi kwa saa za England jana kabla ya kutua Hispania kwa ajili ya vipimo vya afya akitarajiwa kukamilisha dili lake kesho.

Barcelona imefanikiwa kuwashinda Liverpool na Bayern Munich katika mbio za kuwania saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, alikutana na wawakilishi wa Gordon Jumatatu iliyopita, huku Jumatano ikithibitika kuwa klabu hiyo imekubaliana dili la pauni  70 milioni likijumuisha bonasi pamoja na asilimia ya mauzo ya baadaye kwa Newcastle.

GODO 02
GODO 02

Awali, kambi ya Gordon ilikuwa kwenye mazungumzo na Barcelona pamoja na Bayern Munich, ambapo makubaliano binafsi na Bayern yalikuwa karibu kukamilika kwa wiki kadhaa. Hata hivyo, mabosi wa Bayern hawakuwa tayari kuongeza dau lao la pauni milioni 60.

Msimu uliopita, Gordon alikuwa mfungaji bora wa Newcastle baada ya kufunga mabao 18, lakini alikosekana katika mechi sita za mwisho kutokana na sintofahamu kuhusu mustakabali wake.

Kocha Eddie Howe alikiri kuwa tetesi za uhamisho ndizo zilizomuweka nje ya kikosi katika kipindi hicho.

Everton, klabu yake ya zamani, itanufaika pia na dili hilo kwani ina kipengele cha kupata asilimia 15 ya faida baada ya kumuuza Gordon Newcastle kwa pauni milioni 45 mwaka 2023.

Usajili wa Gordon Barcelona unaibua maswali mapya kuhusu hatma ya Marcus Rashford, ambaye ameonyesha kiwango kizuri akiwa kwa mkopo kutoka Manchester United.

GODO 01
GODO 01

Tatizo kubwa lililoonekana kuizuia Barcelona kumsajili Rashford moja kwa moja ni hali ya kifedha, jambo linalofanya wengi kushangazwa kuona klabu hiyo ikitoa fedha nyingi zaidi kwa ajili ya Gordon.

Hata hivyo, Barcelona bado inapanga kufanya mazungumzo na Manchester United wiki hii kuhusu Rashford, huku ikipendelea kuongeza muda wa mkopo wake badala ya kumsajili moja kwa moja.