Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim: Kwa timu hii, bado sana!

Muktasari:

  • Amorim alitapika nyongo baada ya timu yake kupoteza mbele ya Everton iliyobaki na wachezaji 10 na ikapata ushindi wao wa kwanza katika dimba la Old Trafford tangu Desemba 2013.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amekiri kikosi chake hakipo hata karibu kufikia kiwango kinachopaswa kuwa nacho kwa sasa.

Amorim alitapika nyongo baada ya timu yake kupoteza mbele ya Everton iliyobaki na wachezaji 10 na ikapata ushindi wao wa kwanza katika dimba la Old Trafford tangu Desemba 2013.

Baada ya kupoteza mechi hiyo, Man United ilipoteza nafasi ya kupanda hadi nafasi ya tano kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya kutoka sare mechi mbili zilizopita dhidi ya Nottingham Forest na Tottenham.

Amorim alikiri wazi mechi tano timu hiyo ilizocheza bila ya kupoteza haikuwa kwa sababu wamejipata katika mifumo bali ilikuwa ni bahati tu.

"Ninajua tulipo kwa sasa. Daima nimekuwa nikisema hivyo. Hatujafika, wala hatuko karibu hata na kiwango tunachopaswa kuwa nacho ili kupigana katika nafasi za juu za ligi. Tuna mengi ya kufanya na tunahitaji kufanya vitu kwa usahihi zaidi  ili kushinda mechi. Leo (juzi) hatukuwa hivyo. Katika wiki hizi tano kila mtu anatusifu kwa maendeleo yetu. Mimi nasema bado mambo ni yaleyale. Hatujafikia hata ukaribu wa kiwango ambacho klabu hii inapaswa kuwa."

Kwa sasa Man United inashikilia nafasi ya 10 na Amorim ana wasiwasi timu inaweza kurudi na kuwa na matokeo kama ya msimu uliopita.

"Ninahofia kurudi kwenye hali ya msimu uliopita. Hilo ndilo linalonitia wasiwasi zaidi.

Tunahitaji kufanya kazi pamoja na tutafanya kazi pamoja kuhakikisha tunabadilisha hiki kinachoendelea.

Kiungo wa Everton, Idrissa Gueye alitolewa nje dakika ya 13 kwa kumpiga kofi beki mwenzake Michael Keane, lakini bado hiyo haikuisaidia Man United kuibuka na ushindi katika mechi hiyo.