Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim alilia bahati ya Arteta

BAHATI Pict

Muktasari:

  • Arteta amekuwa kwenye benchi la ufundi la Arsenal tangu Desemba 2019 na amekuwa akiungwa mkono na mabosi wa timu hiyo kwa muda wote huo, licha ya kushinda taji moja tu, Kombe la FA kwenye msimu wake wa kwanza.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amedai kwamba anahisi hatapewa muda wa kutosha wa kuijenga timu hiyo kama ambavyo Mikel Arteta amepewa huko Arsenal.

Arteta amekuwa kwenye benchi la ufundi la Arsenal tangu Desemba 2019 na amekuwa akiungwa mkono na mabosi wa timu hiyo kwa muda wote huo, licha ya kushinda taji moja tu, Kombe la FA kwenye msimu wake wa kwanza.

Wakati sasa Arsenal ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na inaelekea kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Man United yenyewe ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi baada ya kukumbana na mfululizo wa matokeo mabaya.

Na kitu pekee ambacho Man United ilichobakiza cha kupambania msimu huu ni Europa League na kocha Amorim alidai imani iliyokuwa imewekwa kwa Arteta kwenye kikosi cha Arsenal hakitafanywa na bilionea Sir Jim Ratcliffe kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

Arteta alibadili utamaduni wa Arsenal, kitu ambacho Amorim anajaribu kukifanya, lakini Mreno huyo mwenye umri wa miaka 40 anaamini hatapewa muda wa kutosha kufikia malengo yake makubwa kwenye klabu hiyo ya Old Trafford.

Amorim, ambaye kikosi chake cha Man United kitakabiliana na Arsenal leo Jumapili, alisema: “Sioni hiyo kitu. Nitapewa muda kama wa Arteta. Nahisi hilo. Hii ni klabu tofauti. Nadhani ni klabu tofauti. Nadhani kutokana na hilo, kwa namna Arteta alivyofanyiwa, alipata muda wa kumvutia kila mtu, lakini mimi sitapewa muda kama ambao Arteta alipatiwa.”

Kocha Amorim alisema wiki za hivi karibuni kwamba anaamini yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza Man United kufikia kwenye malengo makubwa, lakini amekiri matokeo inayopata timu hiyo yatashikilia kibarua chake. Man United imepoteza mechi tano kati ya saba za mwisho ilizocheza kwenye EPL uwanjani Old Trafford na itakuwa na kibarua cha kuikabili Real Sociedad kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya Europa League, ambayo ni mechi muhimu kwao kuliko ya Arsenal.

Kushinda ubingwa wa Europa League ndiyo njia pekee ya United kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kutupwa nje kwenye Kombe la FA.