Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyetajwa nyota ajaye Soton afariki kiutata

Muktasari:

  • Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na klabu yake ya zamani ya Royal Antwerp ya Ubelgiji ikieleza kuwa nyota huyo alifariki dunia mjini Abuja.

ANTWERP, UBELGIJI: ALIYEWAHI kutajwa kama mmoja wa vipaji vinavyochipukia katika mfumo wa vijana wa Southampton, Victor Udoh, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 21 katika mazingira yanayoelezwa kuwa ya kutatanisha nchini kwao, Nigeria, huku ikihusishwa na sumu kwenye chakula au pombe.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na klabu yake ya zamani ya Royal Antwerp ya Ubelgiji ikieleza kuwa nyota huyo alifariki dunia mjini Abuja.

Katika taarifa hiyo, Royal Antwerp ilisema: “Kwa huzuni kubwa, RAFC imepokea taarifa za kifo cha mchezaji wetu wa zamani Victor Udoh. Fikra zetu ziko pamoja na familia, marafiki na wapendwa wake. Tunawapa pole na faraja katika kipindi hiki kigumu sana. Pumzika kwa amani, Victor.” Udoh alipata nafasi yake ya kwanza ya kucheza soka la kulipwa akiwa Royal Antwerp 2019 akicheza mechi 28, ingawa hakufunga bao akitoa asisti mbili za mabao.

Licha ya takwimu hizo, kiwango chake kilivutia macho ya Southampton ambayo wakati huo ilikuwa ikicheza Ligi Kuu England iliyomsajili kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akianzia kikosi cha vijana chini ya miaka 21 mwezi Februari 2025. Hata hivyo, hakudumu muda mrefu kwani  Septemba aliachana nayo kwa makubaliano ya pande zote mbili kabla ya kujiunga na SK Dynamo Ceske Budejovice ya Jamhuri ya Czech mwezi uliofuata kwa mkataba wa miaka mitatu.

Nyota huyo aliripotiwa kuwa alikuwa Abuja usiku mmoja kabla ya kifo chake, ambapo alitoka nje na marafiki zake, na alikutwa asubuhi inayofuata. Baadhi ya ripoti kutoka vyombo vya habari vya Nigeria zilidokeza uwezekano wa sumu ya chakula au pombe, ingawa hakuna uthibitisho uliotolewa. Mamlaka za nchi bado hazijatoa maelezo na chanzo halisi cha kifo chake bado hakijathibitishwa.

Habari za kifo chake zimezua huzuni miongoni mwa mashabiki wa soka na watu waliomfahamu, ambapo shabiki mmoja aliandika: “Miaka 21 ni umri mdogo sana kupoteza maisha. Pumzika kwa amani, Victor.” Mwingine aliandika: “Habari mbaya sana. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.”