Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Hilal ya Sudan yabeba ubingwa Ligi Kuu Mauritania

Muktasari:

  • Al Hilal na Al Merrikh ziliamua kuomba kushiriki Ligi Kuu ya Mauritania baada ya hali ya kiusalama kuwa ndogo huko Sudan. Awali Al Hilal iliomba kucheza Ligi Kuu Bara, lakini kabla ya kupata muafaka ikaibukia Mauritania.

Timu ya Al Hilal ya Sudan chini ya kocha Florent Ibenge, iliyokuwa ilishiriki Ligi Kuu ya Mauritania imetwaa ubingwa ikiwa na michezo miwili mkononi 

Al Hilal na Al Merrikh ziliamua kuomba kushiriki Ligi Kuu ya Mauritania baada ya hali ya kiusalama kuwa ndogo huko Sudan. Awali Al Hilal iliomba kucheza Ligi Kuu Bara, lakini kabla ya kupata muafaka ikaibukia Mauritania.

Hilal imetangazwa mabingwa ikiwa imecheza mechi 28 kati ya 30, ikishinda 18, sare 8 na kupoteza mbili ikivuna pointi 62 nyuma ya Nouadhibou iliyocheza mechi 29 na kuvuna pointi 58 ikibakiza mchezo mmoja tofauti ya pointi nne na mabingwa hao.

Hivyo, Nouadhibou hata ikishinda mchezo wa wa mwisho haitaweza kuzifikia pointi ilizonazo sasa Al Hilal.

Al Merrikh iliyotoka pia Sudan hadi sasa ipo nafasi ya sita ikicheza mechi 29 na kuvuna pointi 44 ikibakiza mechi moja kumaliza ligi.

Licha ya timu hiyo kuwa katika msimamo huo,  itaiwakilisha Sudan kwenye mashindano ya klabu ya CAF msimu ujao

Ligi ya Mauritania inachezwa ikiwa na jumla ya timu 16.