Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo England ampa ujauzito binti wa kocha wake

Muktasari:

  • Arblaster anayeichezea Sheffied United aliyopanda na kushuka nayo Ligi Kuu England ametangaza kuwa anatarajia kuwa baba baada ya kumtia mimba binti huyo wa kocha wa kikosi hicho, Chris Wilder.

LONDON, ENGLAND: Kiungo wa Sheffield United, Oliver Arblaster na binti wa kocha wake, Martha Elizabeth Wilder wamethibitisha kuwa wanatarajia kupata mtoto kutokana na uhusiano wao wa kimapenzi uliodumu kwa muda sasa.

Arblaster anayeichezea Sheffied United aliyopanda na kushuka nayo Ligi Kuu England ametangaza kuwa anatarajia kuwa baba baada ya kumtia mimba binti huyo wa kocha wa kikosi hicho, Chris Wilder.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa na mchango mkubwa kusaidia timu yake kujinasua kutoka hatari ya kushuka Championship baada ya kuanza vibaya msimu huu. Hali ya timu hiyo ilibadilika baada ya kocha Ruben Selles kufutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na shujaa wa klabu, Chris Wilder ambaye ndiye baba mzazi wa Martha Elizabeth.

Ingawa kiwango cha timu kimeshuka tena uwanjani na kuzima matumaini ya kufuzu hatua za mtoano (play-off), ari ya mambo katika klabu imechangamka kutokana na habari za Arblaster aliyesaini kuichezea Sheffield United kuanzia Machi 11, 2022, ambaye alitajwa katika chapisho la Instagram la Martha, Jumapili Aprili 13, kuhusiana na suala la ujauzito.

Katika chapisho hilo, Martha aliweka picha yenye maelezo “+1” akionyesha picha sita za maendeleo ya ujauzito pamoja na vipimo, huku akimtaja Arblaster. Ingawa jinsia ya mtoto bado haijajulikana, marafiki na mashabiki walijaza sehemu ya maoni mtandaoni kwa ujumbe wa pongezi, huku baadhi wakidokeza kuwa huenda ni mtoto wa kiume.

Mmoja aliandika: “Hongereni sana Oli na Martha, atakuwa mtoto mzuri sana,” huku mwingine akiongeza: “Nina furaha sana kwa ajili yenu, siwezi kusubiri kumwona.” Mama wa Arblaster, Sarah, naye alionyesha furaha yake akisema: “Atakuwa mtoto anayependwa sana, siwezi kusubiri kuwa bibi yake.”

Wakati huohuo, Tai Sodje mchezaji mwenzake aliandika Arblaster: “Hongera rafiki yangu.” Mbali na wanafamilia, wachezaji wenzake kama Femi Seriki na Louie Marsh pia waliwapongeza wawili hao kwa habari hiyo ya kufurahisha. Arblaster alikosa nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu uliopita baada ya Sheffield United kufungwa na Sunderland katika fainali ya mchujo (play-off) kwa bao la dakika za mwisho.

Baada ya kipigo hicho, kocha Chris Wilder alifutwa kazi kwa ukali wiki chache tu baada ya mchezo huo wa Wembley. Hata hivyo, kutokana na mwanzo mbaya wa mrithi wake, Selles aliyepoteza mechi zote sita alizoongoza, Wilder alirejea tena kuinoa timu hiyo kwa mara ya tatu.

Arblaster amecheza mechi 17 za Championship hadi sasa akiwa na kikosi hicho baada ya kurejea uwanjani Desemba kufuatia jeraha la goti.