Tetemeko lamvuruga jembe Starlets

TETEMEKO la ardhi lililotokea jijini Marrakech, Morocco wiki iliyopita, limemathiri kisaikolojia straika wa timu ya taifa ya wanawake ya Harambee Starlets, Violet Nanjala anayekipiga na Club Municipal de Laayoune inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Morocco.
Eneo analoishi Nanjala ya Laayoune iko umbali wa kilomita 864.7 kutoka Marrakech ambapo tetemeko hilo liliyokea na watu takriban 2,000 wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine maelfu wakijeruhiwa vibaya.
Nanjala hakuelewa nini kilichotokea kutokana na lugha kugongana sababu taarifa zilikuwa zinakuja kwa Kiarabu hivyo kuwasaka wachezaji wenzake kumpa maelezo ya kina.
“Nilikuta simu nyingi kutoka kwa watu wa nyumbani na hiyo sio kawaida, sikujua kilichotokea hapo awali hadi nilipopitia meseji zote. Watu wa hapa wanazungumza Kiarabu ambacho mimi sikijui. Sisi wachezaji tunaishi katika vyumba tofauti katika makazi ya klabu,” alisema Nanjala.
Straika huyo ambaye yupo katika kikosi cha Starlets chini ya kocha Beldine Odemba kikijiandaa kuwavaa Indomitable Lionesses ya Cameroon gemu ya kufuzu Kombe la Afrika Wanawake, alisema hali hiyo ilimpa uoga hivyo kushindwa kukaa pekee yake.