Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rudisha atamani Wanyonyi azipiku rekodi zake

Rudisha Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye ndoto zake za kuendelea kuweka na kuvunja rekodi mbalimbali zilikatizwa na majeraha, alisema atafurahi kuona rekodi hiyo ikivunjwa katika maisha yake.
  •  

MWANARIADHA David Rudisha anayeshikilia rekodi ya dunia ya mita 800 ameweka wazi anaamini Mkenya mwenzake, Emmanuel Wanyonyi anaweza kuvunja rekodi yake hiyo.
 
Rudisha anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 800, aliyoiweka kwenye michezo ya Olimpiki ya London 2012 alipokimbia muda wa kawaida wa saa 1:40.91 na haijawahi kuvunjwa kwa takribani miaka 12 sasa.

Akihojiwa na chombo cha habari cha Nation, Rudisha amefunguka anaamini rekodi hiyo ipo siku itavunjwa tena kwa siku za hivi karibuni licha ya kuonekana si rahisi.

Mshindi huyo mara mbili wa medali ya dhahabu ya Olimpiki ametaja sifa tatu alizonazo mwanariadha mwenzake Wanyonyi zinazomfanya aamini zitamsaidia kuvunja rekodi hiyo.

"Wanyonyi alikimbia 1:41.11 mwaka jana, sawa na alama ya Wilson Kipketer mwaka 1997, na ana uwezo kwa sababu ya kasi yake, uvumilivu na ujasiri wa kukimbia mbele," amesema Rudisha.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye ndoto zake za kuendelea kuweka na kuvunja rekodi mbalimbali zilikatizwa na majeraha, alisema atafurahi kuona rekodi hiyo ikivunjwa katika maisha yake.

“Sijawahi kuona mtu akivunja rekodi ya dunia, hata Kipketer sikuona hadi nilipokuja kuivunja mwenyewe, hivyo nitafurahi sana kuona mtu akivunja rekodi huku nikitazama jukwaani,” aliongeza. 

Kwingineko, gwiji wa mbio za marathon, Wilfred Bungei pia aliunga mkono maoni ya Rudisha na kumdokeza Wanyonyi kuvunja rekodi hiyo mbele ya mshindani wake mkuu, Marco Arop wa Canada.

Bungei, mshindi wa medali ya dhahabu ya mita 800 katika Olimpiki ya Beijin, China 2008 anaamini ni suala la muda tu kabla ya rekodi ya mita 800 kuvunjwa.