Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamzo aifanya Gor, aapa kuwabeba Police

Mastaa Gor kuhepea Police

UTAKUWA umewahi kuisikia ile kauli ya mbaya wako kaja. Sasa ndicho Gor Mahia walichokutana nacho wikendi hii baada ya kocha waliyemtimua Sammy Pamzo Omollo kurejea na kuwapa kichapo kizito alipowaongoza Police FC.
Baada ya mfululizo wa matokeo duni ndani ya mechi 21, wageni kwenye ligi kuu Police FC waliamua kumtimua kocha Bobby Ogolla wiki iliyopita, aliyewahi pia kuwa naibu kocha wa Gor, kwa kuhofia kushushwa daraja.
Uongozi ulichukua uamuzi huo kwa kuhofia hasara kubwa ya kushusha daraja kwenye msimu wao wa kwanza wa ligi kuu, hasa baada ya kufanya usajili mzito. Baadhi ya nyota waliosajili ni kama vile Francis Kahata, Musa Mohammed, Elvis Rupia, John Makwatta, Harun Shakava, John Ochieng kati ya wengine.
Baada ya kumtupa nje Ogolla na virago vyake , walimteua Pamzo ambaye alichujwa na Gor Januari mwaka huu alikohudumu kama naibu kocha chini yake kocha Mark Harrison.
Sasa baada ya kuanza kazi kwa kushinda mechi yake ya kwanza tena dhidi ya Gor, Pamzo ameapa kuwaboresha Police lakini hata zaidi kuhakikisha wanamaliza kwenye nafasi salama msimu huu.
"Kikosi nilichoridhi kina baadhi ya wachezaji  bora sana kwenye ligi hii wenye uwezo wa kuiokoa klabu. Kinachohitajika ni kuelewa jinsi ya kuwatumia vizuri na naamini ninayo tajriba hiyo. Kazi ya ukocha ni ufahamu na uzoefu. Kwenye mechi yangu ya kwanza nilifanya mabadiliko kwa misingi hiyo na ninakuahidi tutasumbua sababu kuwapiga Gor sio jambo dogo," Pamzo anasema.
Kwenye mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Moi, toka mwanzo hadi mwisho Police FC ndio walionyesha kiwango wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara.
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa Police toka Januari 15, ushindi ambao umewapaisha hadi nafasi ya 10 kwenye msimamo wa jedwali wakiwa na alama 27