OLUNGA: QATAR BADO IKO CHINI

Monday March 29 2021
OLUNGA PIC
By Thomas Matiko

NAHODHA mpya wa Harambee Stars Miachel Olunga kadai kuwa Ligi Kuu ya Qatar aliyojiunga nayo Januari mwaka huu, haina ushindani mkubwa kama ule wa Japan.
Olunga ambaye kwa mara ya pili aliwaongoza Stars akiwa kama nahodha wao kwenye mechi dhidi ya Togo, kasema kuwa ligi kuu ya soka huko Qatar ipo chini na wala hawezi kuilinganisha na ile ya J1 league ya kule Japan alikoshiriki kwa miaka miwili.
“Nimejiunga na Al-Duhail kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Qatar nab ado sijapata fursa ya kucheza dhidi ya timu zote. Ila cha wazi ni kuwa ligi kuu ya J1 ina ushindani mkubwa kuliko wa Qatar Stars League. J1 ni moja kati ya ligi bora Barani Asia kama sio bora.” Olunga anasema.
Licha ya kujiunga na ligi hiyo ya Miliki za Kiarabu msimu ukiwa unakaribia kuisha, Olunga kafanikiwa kucheka na nyavu mara saba kutokana na jumla ya mechi 12 kwenye mashindano yote. Kati ya magoli hayo, matatu alipachika kwenye mechi ya ligi.
Olunga anasema hana hofu kuhusu idadi yake ya magoli kwa sababu bado ni mgeni lakini pia kama alivyotanguliza, ushindani huko Uarabuni sio mkubwa sana.
“Kila ligi huwa na changamoto zake na kule Qatar kuna mazuri na mabaya yake. Bado naendelea kujizoesha na maisha ya kule ila kwenye upande wa ufangujai magoli, hilo nina uhakika idadi itaongezeka. Wala sina shaka na hilo.” Kaongeza.
Alipokuwa Kashiwa Reysol ya Japan, Olunga alipachika magoli 28 kwenye msimu wake wa mwisho kutokana na mechi 32.
Aliishia kutwaa kitau cha dhahabu msimu huo wa 2020 na kuweka historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda golden boot kwenye historia ya ligi hiyo.
Kwa sasa klabu yake ya Al-Duhail ni ya pili kwenye msimamo wa jedwali la ligi ya Qatar Stars League wakiwa na alama 40 baada ya mechi 19. Ligi hiyo imesalia na mechi tatu huku Al Sadd wakiwa na uhakika wa kutwaa taji la msimu huu kwani wanaongoza ligi kuu hiyo kwa alama 50.


Advertisement