Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi Mtendaji CECAFA asimamishwa

CECAFA Pict

Muktasari:

  • Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao cha mashauriano cha marais wa CECAFA kilichohudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama saba wanachama ambavyo ni Burundi, Eritrea, Djibouti, Ethiopia, Tanzania, Kenya na Somalia.

Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wake, Auka John Gecheo, kufuatia uamuzi wa Kamati Tendaji ya baraza hilo.

Katika taarifa iliyotolewa Septemba 22, 2025 na CECAFA, ilieleza: “Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linapenda kuwajulisha wadau kuwa, kufuatia kikao cha Kamati Tendaji kilichoongozwa na Kaimu Rais, Bw. Alexandre Muyenge, na kufanyika kwa njia ya mtandao (Zoom) Septemba 18, 2025, iliamuliwa kumsimamisha Bw. Auka John Gecheo katika wadhifa wake wa Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA.”

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao cha mashauriano cha marais wa CECAFA kilichohudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama saba wanachama ambavyo ni Burundi, Eritrea, Djibouti, Ethiopia, Tanzania, Kenya na Somalia.

Taarifa hiyo pia ilisisitiza dhamira ya baraza hilo kuendeleza uwazi na uwajibikaji, ikieleza: “CECAFA inathibitisha kujitolea kwake kuendeleza maadili ya taasisi hii na itatoa taarifa zaidi kuhusiana na suala hili katika wiki zijazo.”

Kusimamishwa kwa Gecheo, ni mtikisiko mkubwa wa kiuongozi ndani ya CECAFA, huku wadau wakisubiri ufafanuzi zaidi juu ya sababu za uamuzi huo na mwelekeo mpya.

Auka amehudumu katika nafasi hiyo tangu alipoteuliwa mwezi Julai 2020, alipomrithi Nicholas Musonye, aliyekuwa Katibu Mkuu.