Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dabi ya Mashemeji kupigwa Tanzania, Uganda

Muktasari:

  • Hatua ya kiongozi huyo inajiri baada ya kuibuka mzozo mkubwa ukionyesha mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani, huku uwanja ukiwa katika marekebisho yanayoendelea tangu Novemba 29, 2023 kwa ajili ya michuano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.

MWENYEKITI wa AFC Leopards, Dan Shikanda amesema iwapo mchezo wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) dhidi ya Gor Mahia unaotambulika kwa jina la 'Mashemeji Derby', uliopangwa kuchezwa Jumapili ya Machi 2, utashindikana kupigwa nchini humo basi ukachezwe kati ya Tanzania au Uganda.

Hatua ya kiongozi huyo inajiri baada ya kuibuka mzozo mkubwa ukionyesha mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani, huku uwanja ukiwa katika marekebisho yanayoendelea tangu Novemba 29, 2023 kwa ajili ya michuano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.

Shikanda, amesema kwa vile wao ndio wenyeji wa mchezo huo mkubwa unaosubiriwa kwa hamu, amependekeza kwa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) kuupeleka ukachezewe Tanzania au Uganda, ikiwa suala la uwanja uliotangazwa jana Jumanne litakuwa halijafikiwa muafaka.

"Hatutacheza Kasarani na hatuwezi kukubali ratiba hiyo ichezwe Dandora au Kenyatta huko Machakos, kwa sababu viwanja hivyo haviwezi kuhimili ukubwa wa mchezo huo ambao umepangwa kuchezwa Jumapili, kiufupi hadi sasa hatujui tutachezea wapi."

Mwenyekiti huyo alisema wanaweza kutumia Uwanja wa Nyayo ingawa hadi itakapoamuliwa na Kamati ya Ndani ya CHAN, japo wao kama timu mwenyeji wataendelea kusubiri na ikiwa hakuna uwanja utakaokidhi mchezo huo uahirishwe au uchezwe Tanzania au Uganda.

Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Novemba 23, mwaka jana ila uliahirishwa kutokana na ukosefu wa uwanja kwani viwanja vyote viwili vya Kimataifa wa Michezo wa Moi na ule wa Nyayo vinavyoingiza mashabiki 60,000, vimefungwa kwa ukarabati.

Hata hivyo, licha ya mchezo huo kutaka kuchezwa uwanja wa ndani bila ya mashabiki, imepingwa vikali na timu zote mbili, huku mbali na kipute hicho kinachotarajiwa kupigwa Jumapili ila raundi ya pili imepangwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu.

Katika Ligi Kuu ya Kenya, KPL AFC Leopards inashika nafasi ya tano na pointi 34, baada ya kushinda michezo tisa, sare saba na kupoteza mitano, huku Gor Mahia ikishika ya tatu na pointi 36, ikishinda 10, sare sita na kupoteza pia mitano.

Timu zote mbili zimecheza michezo 21 hadi sasa huku, vinara Police FC yenye pointi 41, baada ya kushinda 11, sare minane na kupoteza mitatu, huku Tusker FC ikiwa ya pili na pointi zake 39, ikishinda 11, sare sita na kupoteza minne.