CORONA YATIBUA MATIZI YA BANDARI FC

Tuesday March 30 2021
bandari pic

MOMBASA. TIMU ya Bandari FC haikuonekana ikifanya mazoezi yake ya kawaida huenda kwa sababu ya kusitishwa kwa michezo kiutokana na amri iliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta ya kusimamisha michezo.
Mwanaspoti ilipowasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Bandari FC wa Mbaraki Sports Club, hakukuwa na wachezaji wowote uwanjani siku za Jumamosi na jana Jumatatu, hii ikithibitisha kuwa mazoezi hayakuwako.
Lakini juhudu za Mwanaspoti za kutafuta maofisa wa klabu hiyo kuzungumzia juu ya jambo hilo, ziligonga ukuta kwani simu za Ofisa Mkuu (CEO), Edward Oduor na Meneja wa timu hiyo, Albert Ogari hazikupatikana.
Timu ya Bandari ndiyo ya pekee kutoka jimbo la Pwani inayoshiriki kwenye Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) na wakati huu chini ya mkufunzi wake Mrwanda, Andre Cassa Mbungo, timu hiyo inafanya vizuri.
Kusitishwa kwa ligi hiyo huenda kukawa ni sahali kwa timu tatu zinazoshiriki Supaligi ya Taifa za Modern Coast Rangers na Coast Stima FC ambazo zinakubwa na matatizo ya kifedha kwa ajili ya safari za mechi zao za ugenini.
Rangers ina sahali ya kuwa na usafiri wa bure kutoka kwa kampuni ya basi ya Modern Coast hali Stima imekuwa ikijivutavuta kwa kufanya safari za taabu na ingawa maofisa wao wanafanya juhudi za kutafuta wadhamini, hawajafanikiwa.
Mashabiki wa soka wa jimbo la Pwani wanahuzunishwa na jinsi viongozi wao wa kisiasa wanavyokosa kuzisaidia timu ambazo zinaweza kufanya vizuri na hata kupanda hadi ligi kuu. “Inasikitisha kuwa viongozi hata hawajali timu zetu zikibanduliwa ligini,” amesema shabi Omari Salimu wa Ukunda.

Advertisement